Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Balozi Buzalski katika uzinduzi katika kituo cha afya cha Maganzo

14.06.2021

Tarehe 11 Juni, 2021 Balozi Krzysztof Buzalski alishiriki katika uzinduzi wa mrengo mpya wa kituo cha afya kinachoendeshwa na Shirika la Masista wa Kipolishi Elizabethan Maganzo mkoani Geita. Shukrani kwa mradi uliotekelezwa na Masista kwa ushirikiano na shirika la Redemptoris Missio, unaofadhiliwa na msaada wa Poland, iliwezekana kujenga na kuandaa kituo cha X-ray na ultrasound pamoja na ofisi za madaktari bingwa. Mradi huo ulitekekezwa kama sehemu ya kampeni ya Polonia kwa majirani na usaidizi wa Kipolandi kwa mskini zaidi walioathiriwa na janga la virusi vya korona.

Maganzo 2021_2

Maganzo iko katikati ya eneo la Geita eneo lenye dhahabu kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Uchimbaji wa dhahabu na wachimbaji maskini unafanywa kwa njia rahisi, mara nyingi hatari kwa afya, katika mazingira ya vumbi na kwa matumizi ya zebaki yenye sumu. Matokeo yake ni visa vingi vya magonjwa ya mfumo wa upumuaji na uwezekano fulani wa virusi kama vile UVIKO-19. Mradi wa msaada wa poland utaruhusu massiter wa Maganzo na kliniki inayoendeshwa nao kutambua magonjwa haraka na kusaidia wale wanaohitaji. Kwa kufanya hivyo tunachangia afya za wananchi maskini wa mkoa wa Geita.

Picha (3)

{"register":{"columns":[]}}