Habari
-
09.10.2021Msaada wa Poland kusaidia uwezeshwaji wa muingiliano wa maisha ya binadamu na tembo katika Bonde la Kilombero nchini TanzaniaKatika ratiba ya utendaji kazi wa msaada wa Kipoland, Ubalozi wa Jamuhuri ya Poland Dar es Salaam unawezesha hatua za shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kazi kwa manufaa ya kuboresha muingiliano wa kimaisha wa watu na tembo katika Bonde la Kilombero. Lengo ni kutafuta ufumbuzi katika eneo la mwingiliano wa kimaisha baina ya wanyama na jamii ya wenyeji, kwa kuzingatia tatizo linalosababishwa na upanuzi wa makazi ya watu na kilimo kwenye maeneo ambayo wanyama hao wapo, kwa mfano kando kando ya mipaka ya maeneo hifadhi.
-
23.09.2021Kituo cha huduma cha St. Angel Day Care na basi jipya la shule lililofadhiliwa na msaada wa PolandBasi jipya la kituo cha kulelea watoto cha St. Angel Day Care kilichopo Kurasini, Dar es Salaam, limenunuliwa katika mfumo wa mradi wenye kichwa kisemacho “kuongeza fursa za elimu kwa watoto kurasini kwa kusaidia vyombo vya usafirishaji” kwa wengine kutoka katika mfuko wa misaada wa Poland.
-
20.09.2021Tunajiunga na Siku ya Usafi Duniani nchini TanzaniaJumamosi Septemba 18, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam kwa mara nyingine ulijiunga na Siku ya Usafi Duniani nchini Tanzania.
-
08.09.2021Wanafunzi kumi na mbili wa Kitanzania kupatiwa udhamini chini ya programu ya BanachBalozi Krzysztof Buzalski na Konsul Piotr Kruze walikutana Septemba 8, 2021, kundi la wanafunzi wenye bahati kutoka Tanzania waliotunikiwa chini ya programu ya Banach, mpango wa pamoja wa Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Elimu na Sayansi na Wakala wa Taifa wa Poland wa ubadilishano wa Kitaaluma. Programu imeelekezwa kwa vijana kutoka katika nchi zinazoendelea ambao wangependa kuchukua masomo ya shahada ya udhamili nchini Poland.
-
16.07.2021Ubalozi ukiwasaidia wasanii wa Poland wakati wa Tamasha la Pamoja ZanzibarKatika nusu ya kwanza ya Julai 2021, tulipata furaha kuwakaribisha kundi la wasanii wa Poland waliotumbuiza wakati wa mfululizo wa matamasha kama sehemu ya Tamasha la Pamoja Zanzibar, lililoandaliwa na Radek Bond Bednarz, msanii na mtayarishaji wa Poland, mwanzilishi wa Eklektik jukwaa la kitamaduni, linalojulikana kwa shughuli zake huko Wraclaw.
-
28.06.2021Naibu Waziri Paweł Jabłoński atembelea Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMaendeleo yenye tija baina ya nchi zote mbili na matarajio ya kuimarishwa, katika nyanja zote mbili za kisiasa na kiuchumi, zilikuwa ni mada za ziara ya Naibu Waziri Paweł Jabłoński katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnano Juni 22 -24, 2021
-
14.06.2021Balozi Buzalski katika uzinduzi katika kituo cha afya cha MaganzoTarehe 11 Juni, 2021 Balozi Krzysztof Buzalski alishiriki katika uzinduzi wa mrengo mpya wa kituo cha afya kinachoendeshwa na Shirika la Masista wa Kipolishi Elizabethan Maganzo mkoani Geita. Shukrani kwa mradi uliotekelezwa na Masista kwa ushirikiano na shirika la Redemptoris Missio, unaofadhiliwa na msaada wa Poland, iliwezekana kujenga na kuandaa kituo cha X-ray na ultrasound pamoja na ofisi za madaktari bingwa. Mradi huo ulitekekezwa kama sehemu ya kampeni ya Polonia kwa majirani na usaidizi wa Kipolandi kwa mskini zaidi walioathiriwa na janga la virusi vya korona.
-
05.05.2021Tuliadhimisha kumbukumbu ya miaka 230 ya katiba ya Mei 3 na siku ya wageni wa PolandiWakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani za ubalozi wa Poland jijini Dar es salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alikumbuka historia ya Katiba ya Mei 3 na kusoma barua kutoka kwa Waziri Zbigniew Rau na kuwatakia Poles.
-
03.05.2021Katiba ya Mei 3, 1791Katiba ya Mei 3, 1791 (Sheria ya Serikali) ilipitishwa na Bunge la Poland (Sejm) Mei 3, 1791 ambalo lilikuwa katika kikao tangu 1788, ambayo katika historia ya Poland inajulikana kama Bunge la Miaka Minne au Bunge Kuu.
-
20.11.2020Balozi Krzysztof Buzalski amepata cheti rasmi cha KiswahiliMnamo tarehe Oktoba 20, 2020 Mheshimiwa balozi alifika Baraza la Kiswahi la Taifa la Tanzania (BAKITA) kwa ajili ya kufanya mtihani wake. Baada ya mtihani aliweza kupata ufaulu wa juu yaani daraja la kwanza.