Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Katiba ya Mei 3, 1791

03.05.2021

Katiba ya Mei 3, 1791 (Sheria ya Serikali) ilipitishwa na Bunge la Poland (Sejm) Mei 3, 1791 ambalo lilikuwa katika kikao tangu 1788, ambayo katika historia ya Poland inajulikana kama Bunge la Miaka Minne au Bunge Kuu.

20210503_zdjęcie_3 Maja

Sheria ya serikali ilikuwa ni sheria ya kwanza ya msingi ya Poland na moja kati ya katiba za kwanza duniani kupitishwa katika namna ya mfumo kamili wa kidemokrasia. Nyaraka hizo zilijumuisha utangulizi na vifungu 11. Sheria ya serikali ya Poland ilitambulisha mfumo wa Kifalme ambao katika karne iliyofuata tu ulikuja kutungwa na nchi nyingi za Ulaya.  Mei 3, 1791 Katiba iliendeleza mfumo wa kijamii wa kidaraja (estates), lakini ilifungua njia kwa maendeleo ya kijamii na mitazamo kwa marekebisho zaidi ya kimfumo. Katiba iliukubali mgawanyo wa kimadaraka wa Mfaransa maarufu Montesquieu tripartite katika bunge, serikali na mahakama.

Bunge Kuu, ambalo lilifanikiwa kuunda muungano wa mihimili ili kuepuka mwingiliano, kwa kiwango kikubwa yote ilikuwa ni matokeo ya juhudi na mawazo ya Sheria ya  mfalme Stanislaw August. Mfalme mwenyewe na wanasiasa maarufu Ignacy Potocki na Hugo Kollataj walikuwa ni waandishi wakuu wa sheria ya Serikali.

Bunge Kuu la Sejm (Miaka Minne) (1788 – 1792), ambalo lilipitisha Sheria ya Serikali, lilianza vikao vyake katika hali ngumu ya kimataifa. Urusi ambayo ilikuwa na uanagalizi kamili juu ya Jumuia ya madola ya Wapoland-Walithuania, ilikuja kuingizwa katika vita, na Prussia ilichukua nafasi kiuwazi kinyume na Urusi. Ilionekana kuwa fursa pekee ya kurejesha uhuru wa Poland. Sejm lilifanikiwa kuunda mihimili ya muungano, na kile kilichoitwa mkataba wa dhamana (treaty of guarantee) kilikomeshwa, na kufuatiwa na mvunjiko wa Baraza la kudumu (Perpetual Council), Sejm lilichukua mamlaka yote katika nchi, kuanza kwa jaribio la kuunda upya mfumo. Upitishaji wa Sheria ya Serikali ulikuwa ni hatua za kilele cha shughuli hizo. Urusi haikuwahi kukubali kupoteza ushawishi wake katika Poland, na baada ya kusaini mikataba ya amani na Uturuki na Sweden, vitendo vya kijeshi vilianza dhidi ya Jumuia ya madola. Muda mfupi hayo yalipelekea kujisalimisha kwa mfalme na mamlaka ikachukuliwa na wapinzani wa katiba ya Mei 3, 1791, ambao waliungana katika mhimili ulioundwa chini ya ushawishi wa Urusi, ulioitwa Mhimili wa Targowica kutokana na mji ambao ulianzishiwa rasmi.

Mara tu baada ya utungwaji wa katiba ya Mei 3, ilitamaniwa na Ulaya nzima. Edmund Burke (1729 – 1797), mwanzilishi Mwingereza wa filosofia ya ubinafsi, aliisifu kama mfano wa mabadiliko ya amani ya mfumo wa siasa. Nyaraka hii iliibua maoni hasi kutoka kwa “Nouvelles Extraordinaires de Divers Endroits” pia. Maneno ya kusifiwa pia yalisikika katika makazi ya Vienna. Papa Pius VI (1775 – 1799) aliichukulia vyema; hata mfalme wa Prussia, Friedrich Wilhelm II (1786 – 1797), alituma barua ya pongezi. Halafu - balozi katika Paris na baadaye Raisi wa Marekani (1801 – 1809), Mwanademokrasia Thomas Jefferson, aliandika kwamba dunia imepata kumbukumbu na heshima ya katiba tatu za heshima katika mpangilio wa utungwaji wake: Katiba ya Marekani, Poland na Ufaransa.

{"register":{"columns":[]}}