Kituo cha huduma cha St. Angel Day Care na basi jipya la shule lililofadhiliwa na msaada wa Poland
23.09.2021
Basi jipya la kituo cha kulelea watoto cha St. Angel Day Care kilichopo Kurasini, Dar es Salaam, limenunuliwa katika mfumo wa mradi wenye kichwa kisemacho “kuongeza fursa za elimu kwa watoto kurasini kwa kusaidia vyombo vya usafirishaji” kwa wengine kutoka katika mfuko wa misaada wa Poland.
Mradi umetekelezwa kwa ushirikiano wa Usharika wa ‘Marry Immaculate Sisters’ unaofanya kazi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam na MIVA(Mission Vehicle Association). Kazi ya Shirika la Masista wa Maria Immaculate nchini Tanzania imejikita katika kufanya ziara za nyumbani, msaada wa kichungaji, kufundisha katekisimu katika shule za sekondari na kuendesha shule za chekechea, pia na masista wa Poland.
Kituo cha Kulelea watoto cha St. Angel Day Care kilichotembelewa tarehe Septemba 23, mwaka 2012 na mwakilishi wa ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaa, Katarzyna Sobiecka, kilianza shughuli zake Januari 2007. Kinapokea watoto bila kujali asili zao, hali yao ya kijamii, au imani (takribani wanafunzi 80 wenye umri wa miaka 3 hadi 6). Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika kituo hiki cha elimu husafiri kutoka wilaya za mbali za Dar es Salaam, ambako ubora wa barabara unasababisha ugumu wa kusafiri- kiasi kwamba baadhi ya maeneo huwezi kutembea wakati wa mvua-na ambapo ni hatari kusafiri kwa usafiri wa umma. Vivuko vilivyoteuliwa vya watembea kwa miguu ni vichache sana
Basi jipya la shule sio kwa ajili tu ya kuhakikisha usalama wa watoto njiani kwenda shule ya chekechea na wakati wa kurudi nyumbani, lakini pia huwasaidia wazazi wao kwa kiasi kikubwa, inasaidia kuboresha mpangilio wa shughuli za shule bila kujali hali ya hewa, na kupunguza gharama za matengenezo ya chekechea.