Mkutano wa Wafanyabiashara wa kutoka Poland na kutoka Tanzania jijini Dar es Salaam
11.06.2024
Mnamo tarehe 18-19 Julai 2024, jijini Dar es Salaam, kwa mwaliko wa Chamba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture - TCCIA), ulifanyika mkutano wa biashara uliandaliwa na Chamba cha Biashara cha Kitaifa cha Poland (KIG) kwa kushirikiana na Chamba cha Biashara na Viwanda cha Mkoa (IPH) cha Bialystok.
Washiriki wa ziara ya biashara kutoka Poland walitoka Chamba ya Biashara cha Kitaifa (KIG), Chamba ya Biashara na Viwanda (IPH) cha Bialystok, Hifadhi ya Sayansi na Teknolojia ya Suwalki, na pia kutoka makampuni kutoka Poland yalizoziwakilisha sekta za kilimo, teknolojia ya habari, taa, utalii, na samani yaani fanicha. Mkutano huo ulifunguliwa na hotuba za Makamu wa Rais wa Chamba ya Biashara, Viwanda na Kilimo cha Tanzania (TCCIA), Bwana Boniface Thomas Ndengo, Makamu wa Rais wa KIG Witold Karczewski, na Rais wa IPH wa Bialystok, Jarosław Antychowicz, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Siasa, Kiuchumi, Kikonseli na Wanadiaspora wa Poland wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka.
Mkutano haukuwa tu fursa ya kuanzisha uhusiano wa moja kwa moja kati ya wafanyabiashara kutoka Poland na kutoka Tanzania, bali pia kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya KIG, TCCIA na IPH, pamoja na Dar es Salaam Chamber of Commerce - DCC.
Sambamba na mkutano, pia yalianzishwa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya mji wa Bialystok na Dar es Salaam, Suwalki na Moshi. Mazungumzo ya ushirikiano pia yalianzishwa kati ya Chuo Kikuu cha Bialystok na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na Hospitali ya Mkoa ya Bialystok na hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Washiriki wa ziara kutoka Poland na wakilishi wa TCCIA, wakiongozwa na rais wa TCCIA, Vincent Bruno Minja, walipokelewa katika Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, ambapo pande zote mbili zilithibitisha mazungumzo ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili.