Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Naibu Waziri Paweł Jabłoński atembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

28.06.2021

Maendeleo yenye tija baina ya nchi zote mbili na matarajio ya kuimarishwa, katika nyanja zote mbili za kisiasa na kiuchumi, zilikuwa ni mada za ziara ya Naibu Waziri Paweł Jabłoński katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnano Juni 22 -24, 2021

MF 2021_1

-Poland inaichukulia Tanzania kuwa washirika wa msingi katika bara la Afrika, ni miongoni mwa nchi nne za kipaumble kusini mwa Jangwa la Sahara kama sehemu ya ushirikiano katika maendeleo. Tungependa kukuza uhusiano wa karibu zaidi, hasa katika nyanja ya uchumi - alisisitiza Naibu Waziri Jabłoński wakati wa mkutano na wadau wake wa Tanzania, Naibu Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mbarouk Nasser Mbarouk.

Mbali na mazungumzo katika MFA ya Tanzania, Naibu Waziri Jabłoński alifanya mazungumzo katika wizara zinazohusika na maeneo muhimu zaidi ya ushirikiano wa Poland-Tanzania.

Mkutano na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Elimu Joyce Ndalichako, uliohudhuriwa na wawakilishi wa vyuo vikuu vya Poland na mashirika yasiyo ya kiserikali, ulijikita katika kuelimisha rasilimali watu muhimu kwa maendeleo ya sekta zinazoongoza uchumi wa Tanzania, ikiwemo ushirikiano wa kitaaluma katika eneo la kilimo. Hususani eneo muhimu la ushirikiano huu labda uimarishwaji katika ubadilishanaji wa wanafunzi kutoka katika nchi zote mbili na kuongeza upatikanaji wa ufadhiri wa wanafunzi.  Masuala haya pia yalijitokeza kwenye mkutano wa Naibu Waziri Jabłoński na Bertram Mapunda, msimamizi wa chuo kikuu cha Jordan, kinachowezeshwa kwa msaada wa Poland, na ushirikiano wa wamishonari wa Poland na chou kikuu hiki.

Mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, Waziri wa Biashara na Viwanda Prof. Kitila Mkumbo na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu matarajio na hali ya ushirikiano wa kiuchumi katika namna ya fulsa za uwekezaji kwa makampuni ya Kipoland nchini Tanzania. Wafanya biashara wa Kipoland wako tayari kutoa teknolojia za kisasa, likiwemo eneo la ICT, finitech, maji, miundombinu ya usafi, uchimbaji na uchakataji wa madini na vilevile ulinzi wa mazingira. Kama sehemu ya ajenda ya uchumi. Mwanzoni makampuni ya Kipoland yalitekeleza mikataba kwa mujibu wa mikopo ya serikali katika misaada iliyofungwa suala hili pia lilijadiliwa.

Wakati wa ziara, makamu mkuu wa diplomasia wa Poland pia alikutana na Maryprisca Winfried Mahundi, naibu Waziri wa maji, ambaye alisaini naye makubaliano ya kutambua upana wa kazi  za miradi iliyo chini ya Poland-Tanzania, kuboresha mfumo wa upatikanaji wa maji na ufanisi katika usimamizi wa rasilimali maji, Katika Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi katika Tanzania na mji mkuu wa nchi Dodoma na vilevile kujihusisha katika uimarishaji wa watendaji katika mashirika ya wenyeji. Mradi utatekelezwa kwa ushirikishwaji wa wafanya biashara wa Kipoland kutoka katika ICT na sekta ya maji na vilevile vyuo vikuu.

Naibu Waziri Jabłoński pia alitembelea Wakala wa Mafunzo ya Ufugaji (LITA) Tengeru, yanayowezeshwa na Poland kwa zaidi ya miaka kumi kwa kuongeza weredi wa watendaji kuelimisha wataalam wa afya ya mifugo, kuboresha miundombinu na vitendea kazi na vifaa vya kisasa vya maabara. Ziara pia ilijumuisha kituo cha shirika la APOPO kilichopo Morogoro, kinachohusika na upimaji na utambuzi wa maambukizi ya kifua kikuu na panya wakubwa wa kusini waliochomwa. Shukrani kwa msaada wa Poland, programu ya utambuzi wa kifua kikuu ilienea na kujumuisha baadhi ya hospitali katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.

Makamu kiongozi wa diplomasia wa Poland, pia alitembelea kwenye makaburi ya Wapoland Tengeru (eneo lenye makaburi mengi zaidi katika Tanzania ya raia walioenda uhamishoni wakisindikiza jeshi la Generali Anders), pia alikutana na jamii ya Wapoland na Wamishonari wanaofanya kazi Tanzania.

Ziara ya Naibu Waziri Jabłoński ilisindikizwa na misheni ya uchumi iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje, ikijumuisha wawakilishi wa makampuni ya Kipoland yenye nia ya kuwepo Tanzania.

 

 

 

 

Picha (14)

{"register":{"columns":[]}}