Tunajiunga na Siku ya Usafi Duniani nchini Tanzania
20.09.2021
Jumamosi Septemba 18, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam kwa mara nyingine ulijiunga na Siku ya Usafi Duniani nchini Tanzania.
Mwishoni mwa wiki, wafanyakazi wa ubalozi na familia zao walishiriki katika usafishaji wa Coco Beach jijini Dar es salaam, iliyo karibu na Ubalozi huo. Kampeni hii huandaliwa kila mwaka nchini Tanzania na shirika lisilo la kiserikali la ‘Nipe Fagio’ ambalo mwaka jana pia lilitekeleza mradi unaohusiana na kuchakata takataka (recycling) shukrani msaada wa kifedha kutoka katika mfuko wa msaada wa Poland.