Wanafunzi kumi na mbili wa Kitanzania kupatiwa udhamini chini ya programu ya Banach
08.09.2021
Balozi Krzysztof Buzalski na Konsul Piotr Kruze walikutana Septemba 8, 2021, kundi la wanafunzi wenye bahati kutoka Tanzania waliotunikiwa chini ya programu ya Banach, mpango wa pamoja wa Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Elimu na Sayansi na Wakala wa Taifa wa Poland wa ubadilishano wa Kitaaluma. Programu imeelekezwa kwa vijana kutoka katika nchi zinazoendelea ambao wangependa kuchukua masomo ya shahada ya udhamili nchini Poland.
Mwaka huu, maomba 260 kutoka katika nchi takribani 30 yalichaguliwa miongoni mwa maombi takribani 2000 yaliyotumwa. Vyuo vikuu vinavyochaguliwa mara nyingi na waombaji wanaobahatika kupata nafasi ni Chuo kikuu cha Teknolojia cha Warsaw, Chuo Kikuu cha Warsaw, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Wrocław, Chuo Kikuu cha Wrocław na Chuo Kikuu cha Jagiellonian katika Kraków. Linapokuja suala la mchepuo maarufu wa masomo, wengi wa wanufaika hupenda kusoma Masomo ya Uinjinia na Sayansi ya Ufundi (engineering and technical sciences), Sayansi halisi (exact sciences) na Sayansi ya asili (natural sciences).
‘Udhamini huu ni kwa manufaa makubwa kwani michepuo hii ni muhimu sana kwa mkakati wa maendeleo kwa nchi za kisasa na uwezo wake katika wakati uliopo. Zaidi ya hayo, programu inatuwezesha kuimarisha ushirikiano na nchi sio tu za ukanda wetu bali pia kutoka Asia, Afrika, au Amerika ya Kusini. Shukrani kwa mkakati huo, Poland kwa wakati mwingine imefanyika kuwa daraja kati ya nchi zinazoendelea na Magharibi,’ anasema Dr. Grażyna Żebrowska, Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Taifa wa Poland wa ubadilishano wa Kitaaluma.
Prof. Stefan Banach (1892–1945), ambaye programu hii ilipewa jina lake, ni mmoja wa watu maarufu sana duniani mwanamahesabu wa Kipoland. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Shule ya Hesabu ya Lvov na vilevile uchambuzi wa kisasa wa kazi (modern functional analysis) – tawi la Kihesabu (a branch of mathematics applied) miongoni mwa mengine katika kuelezea mambo ya kiasili (natural phenomena)