Makazi ya Wapoland Tanganyika wakati wa Vita vya Kidunia vya pili
Kufukuzwa kutoka Poland - Mwanzo wa Kutembea Tembea
Mwaka 1940-41 mamia elfu ya raia wa Jamuhuri ya pili ya Poland walifukuzwa katika Sovieti ya Urusi, ikiwa ni matokeo ya uvamizi wa Wanazi wa Ujerumani na kuchukua eneo la Mashariki la Poland baada ya Septemba 17, 1939.
Baada ya uvamizi wa Wanazi wa Ujerumani katika muungano wa Kisovieti na muafaka wa akubaliano ya Sikorski-Maisky Julai 1941, ambapo Poland na Muungano wa Kisoviet walikuwa washirika, mamlaka ya Moscow iliwaruhusu Wapoland kuondoka na kwenda uhamishoni. Makundi yalikwenda kwenye majimbo ya muungano wa Kisovieti ambako ndiko jeshi la Poland lilianzishwa chini ya usimamizi wa kamanda Generali Wladyslaw Anders, akitegemewa katika ulinzi na katika kuondoka kwenye muungano wa Kisovieti pamoja na askari.
Kuhamia Iran
Watu wa Poland, raia na wanajeshi, walihamia Iran kutoka katika muungano wa Kisoviet katika hatua mbili kutoka mwezi Machi hadi mwezi Septemba 1942. Njia kuu ilipitia Turkmenistan kwenda kambi ya Pahlevi transit Iran (ambayo kwa sasa ni Bandar-e Anzali) na kutoka hapo kwenda kuweka kambi Tehran. Baada ya uhamiaji kukamilika kulikuwa na raia wa Poland zaidi ya 110 000 Iran.
Kwa bahati mbaya, kwa sababu ya hali mbaya za kiafya ambayo zilisababishwa na hali duni ya maisha katika muungano wa Kisoviet na ugumu katika kusafiri, zaidi ya watu 2,100 (sawa na asilimia 5.7% ya watu wote) walifariki Iran kwa sababu ya ugonjwa wa Kuhara, homa ya matumbo (Taifodi), Malaria na magonjwa yanayosababishwa na utapiamlo.
Raia wa Poland hawakuweza kukaa Iran kwa muda mrefu kwasababu ya hali nzito ya kimataifa na itisho vya kukera vya Wajerumani. Mipaka ya Poland ilichukuliwa kwa hiyo Serikali ilibaki tu kutegemea msaada wa Waingereza kusaidia kuwatafutia watu makazi. Uingereza ilikubali kuwahamisha raia wa Poland kutoka Iran na iliwasilisha mpango wa sehemu ya makazi ya wakimbizi. Wasafirishaji wa majini walipelekwa katika kambi za usafirishaji Uingereza India (Bandari ya Karachi katika Pakistani ya leo) na kutoka pale kuelekea kwenye makazi India, Afrika, Mexico na New Zealand. Shughuli hii ilikuwa ngumu, ilitumia muda mwingi na iligharimu sana, hasa katika hali ambayo vita vilikuwa vikiendelea.
Wanajeshi wa Poland walitoka Iran na walikwenda Iraq na Palestina ambapo walitakiwa kuwa mstari wa mbele katika vita ya pili ya dunia.
Wakimbizi wa Kipoland katika Afrika
Wimbi kubwa la wakimbizi wa Kipolandi liliondoka na kuelekea Afrika. Julai 1942 Serikali katika London kwa kushauriana na Magavana wa Tanganyika, Kenya, Uganda na Nyasa wa wakati huo walikubaliana kuwahifadhi wakimbizi wa Kipolandi kwa wakati ule wa vita. Pia walizingatia suala la kuwaweka raia wa Poland katika nyazifa ndogo ndogo za uongozi katika Rhodesia ya kaskazini na kusini na katika muungano wa Afrika kusini.
Mapema mwezi Septemba 1941, Serikali ya Poland iliamua kuweka majengo ya mashauri Kenya, Tanganyika na Uganda na vile vile katika Rhodesia zote na katika muungano wa Afrika kusini. Wanadeplomasia pamoja na wajumbe wa Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ilihusika na wakimbizi wa Kipolandi. Mamlaka za Uingereza pia zilikuwa zikijiandaa kuingia Afrika.
Msafara wa kwanza wa kuwasafirisha wakimbizi wa Kipoland kutoka katika Muungano wa Kisovieti ulifika katika bandari ya Tanga Agosti 27, 1942. Watu 1,400 walifika kwa meli, halafu walisafirishwa kwenda Dar es Salaam. Msafara mwingine ulifika bandari ya Mombasa Kenya Septemba 19.
Mwishoni mwa mwezi septemba 1942, watu 1044 walipelekwa katika makazi ya Masindi Uganda, watu 510 walipelekwa Morogogo na watu 401 walipelekwa Kondoa Tanganyika. Makundi yaliyofuata yalifika mwezi Oktoba na yalipelekwa Tengeru, Kondoa , Ifunda na Kidugala.
Nafasi ya wakimbizi wa Kipolandi kuondoka kutoka Iran kwenda Afrika ilikuwa kubwa. Mwishoni mwa 1944 kulikuwa na raia wa Poland 13,364 katika nchi tatu za Afrika mashariki, ambapo 6,331 walikuwa Tanganyika. Mategemeo ya kumalizika kwa vita yalifanya uhamaji kusitishwa. Katika Afrika Mashariki yalianzishwa makazi sita ya kudumu ya wakimbizi wa Kipoland. Manne yalikuwa Tanganyika (Tengeru, Kondoa, Ifunda na Kidugala) na mawili yalikuwa Uganda (Masindi na Koja) mbali na makazi ya kudumu, yalianzishwa makambi kadhaa, ikiwemo katika Morogoro, Kigoma, Dar es Salaam, Iringa na Tosamaganga katika Tanganyika.
Wakati huo lilikuwa ni kundi la wachache kutoka Ulaya walioko Afrika Mashariki.
Maisha katika Makazi
Tengeru yalikuwa ni makazi ya Wapoland ambayo yalikuwa makubwa kuliko yote ambapo yalikuwa na nyumba 947. Kipindi hicho watu 4,018 waliishi katika makazi hayo. Makazi ya Kondoa yalikuwa na watu 430 ambao waliishi katika makambi ishirini yaliyojengwa kwa udongo. Kundi ambalo lilikuwa na makazi bora kuliko yote ni kundi ambalo lilifanya makazi yake Ifunda, watu 780 waliishi katika nyumba 100 za matofali zilizokuwa katika wilaya tano, ambapo zilikuwa na sehemu za majiko, sehemu za kulia chakula, sehemu za kufulia na kupigia pasi nguo na maghala. Katika makazi ya Kidugala, kundi la watu 798 liliishi karibu na makazi yaliyotelekezwa na Wamishenari wa Kiprotestant wa Ujerumani.
Wakazi wa Tanganyika, kwa Juhudi zao wenyewe, waliwasaidia wageni kutoka Poland kuweza kusihi katika nchi mpya. Makabila ya wenyeji yaliyasaidia makundi haya vifaa vya ujenzi na chakula na yalifanya kazi katika ujenzi wa makazi ya Wapolandi.
Kundi la wakimbizi wa Kipolandi pia liliweza kuinuka katika Rhodesia zote na katika Muungano wa Afrika Kusini.
Kiongozi mkuu – kwa kawaida alikuwa Ofisa wa Kiingereza ndiye aliyekuwa mtawala mkuu katika kila makazi. Alisaidiwa na Meneja wa kambi ambaye aliteuliwa na Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ya Polani. Makazi yaligawanywa katika sehemu sehemu na katika makundi, waliteuliwa wakuu wa Idara ya elimu, huduma za ufugaji, huduma za Afya, utamaduni na kazi ili kusimamia. Pia kulikuwa na
mabaraza yaliyowawakilisha wenyeji. Gharama za kudumisha makazi zililipwa na Uingereza kama deni la Serikali ya Poland na Wiraza ya Kazi na Ustawi wa Jamii chini ya Serikali iliyokuwa uhamishoni Londoni.
Makundi yaliyoishi katika makazi ya Tanganyika ya kipindi hicho yaliunda jumuiya zilizopangwa vizuri na zenye ufanisi katika mfumo wa elimu, katika shughuli za utamaduni na michezo. Mashamba pia yaliendeshwa. Watoto na vijana wadogo walipatiwa elimu katika ngazi ya chekechea na huduma za kishule katika ngazi mbalimbali. Wenyeji walishiriki katika vyama mbalimbali vya kiutamaduni na michezo. Skauti ndio mchezo uliojulikana sana. Vyombo vya habari vya Kipoland viliboreshwa (vichwa vikubwa vya habari: “Kundi lililo katika Afrika” na “Sauti ya Poland” na magazeti kadhaa yalichapishwa katika makazi) na hata vipindi vya redio kwa lugha ya Kipolandi vilitandazi kutoka Nairobi.
Kufungwa kwa Makazi
Wakati vita vinakaribia kufika mwishoni na uondolewaji wa kutambuliwa kwa Serikali ya Polandi uhamishoni tarehe 5 Julai 1945 na Uingereza, kuliibua maswali mengi kuhusu mstakabadhi wa makazi ya Wapoland katika Afrika. Makundi yaliyoko Afrika yalikatishwa tama sana na matokeo ya mkutano uliofanyika Yalta ambao ulipelekea Poland kuanza kutegemea utawala wa Joseph Stalin na wao hawakutaka kurudi Polandi kuongozwa na Wakomunisti ambao waliongozwa na mamlaka iliyo chini ya Moscow. Ni kama wakimbizi wa Kipolani 3,800 tu ambao waliamua kurudi nchini sawa na asilimia 20% ya watu wote. Wengi wao walikataa kurudi nchini.
Agosti 1, 1946, wajibu wa kifedha wa matengenezo ya makazi ya Wapoland ulichukuliwa na umoja wa Mataifa katika idara ya misaada na ukarabati (United Nations Administration for Relief and Rehabilitation Administration, UNRRA) na kutoka Julai ulichukuliwa na Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (International Refugees Organization (IRO). Kwa sababu za kifedha iliamuliwa kwamba makazi ya Wapoland yapunguzwe, yalibakizwa mawili tu Tengeru (Tanganyika) na Koja (Uganda).
Novemba 1947, hatua ya kuwaunganisha wanajeshi na familia ilianza shukrani ni kwa watu 9,500 walioondoka Afrika. Mwaka 1948 idadi ya watu ilipungua mpaka kufikia 3,497 ambayo kati yao 2,080 waliishi Tanganyika. Baadhi yao walihamia Marekani, Argentina, Kanada, Ufaransa na Australia. Makazi ya Koja na Tengeru yalihitimisha shughuli zao kwenye nusu ya pili ya 1952. Watu mia kadhaa walibaki Tanganyika. Mtu wa mwisho, Bwana. Edward Wojtowicz alizikwa Tengeru mwaka 2015.