Tanzania
Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Poland na Tanzania ulianzishwa mnamo Januari 1962.
Ushirikiano wa Kisiasa
Mtazamo wa Kihistoria
Mnamo Aprili 1962, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland Dar es Salaam ulianza kufanya kazi. Balozi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyeishi Moscow (tangu 1990 Berlin) alitambulika Poland.
Mnamo mwaka 1987, Waziri wa mambo ya nje Benjamin Mkapa alitembelea Poland.
Katika mahusiano ya Poland –Tanzania, makubaliano yafuatayo yalisainiwa mpaka mwaka 1989.
- Mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Poland na Mtukufu Mtawala wa Uingereza na Ireland Kaskazini, kuhusiana na uhalalishaji wa kuendelea kwa masuala ya uraia na biashara ya Agosti 26, 1931 (iliingia katika utekelezaji Mei 30, 1932);
- Mkataba kati ya Rais wa Jamhuri ya Poland na Mtukufu Mfalme wa Uingereza na Ireland na Milki za Uingereza nje ya mipaka yake, Mfalme wa India, wa wakimbizi wahalifu kujisalimisha wa Januari 11, 1932 (iliingia katika utekelezaji Machi 12, 1934).
-
Mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Poland na Mtukufu Mfalme wa Uingereza na Ireland na Milki za Uingereza nje ya mipaka yake, Mfalme wa India kwa utambuzi wa vyeti vya usajili ulio sawa kwa wote na nyaraka nyingine za kiserikali zinazohusisha upimaji wa uzito wa meli za wafanyabiashara wa Aprili 16, 1934 (iliingia katika utekelezaji Machi 12, 1934).
-
Makubaliano kati ya Serikali ya Watu wa Jamhuri ya Poland na Serikali ya Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ushirikiano katika Sayansi na teknolojia ya Mei 15, 1965 1934 (yaliingia katika utekelezaji siku hiyo hiyo).
Ushirikiano wa kisiasa baada ya 1989
Poland na Tanzania zinashirikishana uzoefu kuhusiana na mabadiliko katika siasa na uchumi. Kuelekea Oktoba na Novemba 1991, mamlaka maalumu kutoka kwenye Tume ya Rais ya Tanzania ilifanya mchanganuo wa utendaji wa mfumo wa vyama vingi. Ikumbukwe kwamba mahusiano ya nchi hizi mbili yalifanyika kwa Waziri wa Mipango na Ubinafsishaji katika idara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bw. Nassoro Malocho mnamo Februari 14-19, 1999 Warswa. N. Malocho (Mhitimu wa chuo kikuu cha Technolojia Warsaw) alifariki Disemba 2002. Kutoka Disemba 29, 1999 hadi Januari 2, 2000, mjumbe maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi kwa jina Krzysztof Śliwiński alienda Tanzania. Safari ililenga kwenye suala la mgogoro wa maeneo ya maziwa makubwa na utatuzi wake. Mnamo Novemba 17-18, 2003, MFA chini ya katibu wa nchi Bogusław Zaleski alifanya ziara ya kikazi kuenda Tanzania. Alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje Jakaya Mrisho Kikwete (baadaye Rais wa Tanzania). Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Rita Mlaki na). Naibu Waziri wa Kilimo Piu Mbawala.
Mei 2004, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Ngazi ya Juu, Salim Ahmed Salim alikaa Poland. Katika miaka ya 1980 alikuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, na kwa mihula mitatu iliyofuata alikuwa (1989 -2001) alikuwa ni katibu mkuu wa Shirika la Umoja wa Afrika. Novemba 19-22, 2013, Rais Jakaya Mlisho Kikwete alihudhulia kilele cha mkutano wa COP-19 Warsaw. Kando ya mkutano huo alifanya mazungumzo rasmi na Rais Bronisław Komorowski. Mnamo 23-25, 2014, Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda na wajumbe maalumu walitembelea Poland (akiwemo Naibu Waziri wa Fedha na Mambo ya Nje). Alishiriki katika mkutano wa Bodi ya Fedha ya Poland na Wawakilishi wa Serilkali (Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Uchumi na Biashara). Alifanya mkutano na wawakilishi wa Makampuni ya Kipoland yanayoshirikiana na Tanzania. Kutoka Aprili 17, 2015, Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Lishe na Vyama vya Ushirika, Stephen Masatu Alikaa Poland. Alikutana na Waziri wa Kilimo Marek Sawicki na alishiriki katika kongamano la Uchumi la Ulaya (EEC)2015 Katowice. Julai, 2016, Radoslaw Domagalski-Łabędzki, chini ya Katibu wa nchi katika Wizara ya Uchumi, alikuwa katika misheni ya kiuchumi Kenya na Tanzania. Septemba 21, 2016, Katika wakati wa awamu ya 71 ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Witold Waszczykowski, Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, alikutana na Augustin Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania. Januari 2017 Joanna Wronecka, Chini ya Katibu wa nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania A. Mahiga katika mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa.
April 2017, Papa Francis alimteua Askofu Mkuu Marek Solczyński Kuwa Balozi wa kitume Tanzania (Mwanzoni alikuwa balozi katika Armenia). Aprili 2018, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland Jacek Czaputowicz, alitembelea Tanzania na rasmi alifungua Ubalozi wa Jamhuri ya Poland Dar es Salaam. Sherehe ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje Augustine Mahiga, Balozi wa Kitume Askofu Mkuu Marek Solczyński na wawakilishi wa jamii ya Poland na Wafanya biashara wa Kipoland. Wakati wa ziara Waziri J. Czaputowicz pia alikuwa na mashauriano ya kisiasa na Waziri A. Mahiga na alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Kitila Mkumbo katika uzinduzi wa ushirikiano wa sekta za nchi zote mbili. Katika mwaka huo huo Tanzania ilitembelewa na Kiongozi mkuu wa baraza la Rais wa Jamhuri ya Poland, Waziri Krzysztof Szczerski. Aliwasilisha mwaliko uliotumwa na Rais Andrzej Duda kwa Rais John Magufuli ili kufanya ziara na kufanya mashauriano na Susan Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya nje. Ushirikiano kati ya Mabunge ya nchi zote mbili pia yalifanyika. Juni 2015, mjumbe kutoka katika bunge la Tanzania alitembelea Poland. Agosti 11, 2015 azimio la ushirikiano wa Poland-Tanzania lilisainiwa kati ya kundi la Maseneta wa Kipoland na kundi la kirafiki la mkutano mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ushirikiano wa Kiuchumi
Poland inasafirisha kuenda Tanzania, vitu kama mashine na vifaa, chakula, bidhaa za shaba, makaratasi, nguo, mataili, na vifaa vya nyumbani. Sisi tunaingiza bidhaa za kahawa, chai, kokoa, tumbaku, pamba na mbegu za mafuta kutoka Tanzania. Mwaka 2018 pia korosho ziliingizwa. Kuongezeka kwa biashara kwa kiasi kikubwa kuliletwa na kusaini kwa makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Poland na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutanua misaada ya mikopo iliyofungwa Septemba 28, 2015, kutoa msaada wa mkopo wa USD ml. 110 kwa ajili ya kufanya kilimo cha kisasa. Ilipelekea kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa Poland kusafirisha vitu kuenda Tanzania, ikiwa ni pamoja na Mashine za kilimo na vifaa vyake, na namna ya kutunza nafaka na mfumo wa usimamizi. Kwa msingi wa makubaliano haya, Makampuni ya Kipoland yalihitimisha mkataba kwa ujenzi wa sehemu ya uundaji wa mashine za kilimo na miundombinu ya utunzaji wa nafaka. Kuongezeka kwa haraka kwa idadi ya watalii kumekuwa na matokeo makubwa katika uchumi wa ushirikiano wa nchi zote mbili.
Katika mwaka 2018 kisiwa cha Zanzibar pekee kilitembelewa na watalii wa Kipoland wanaokadiliwa kuwa 16000 waliotumia ndege ya msimu ya malipo ya moja kwa moja. Utalii unafuatiwa na wafanya biashara wa Kipoland – Sasa hivi kuna dazani za uwekezaji wa Kipoland kisiwani, ambao tayari unafanya kazi na ule ulio katika hatua ya ujenzi, na hii imechukuliana na hoteli za wenyeji. Mbuga za wanyama za Tanzania zilizo kaskazini mwa Tanzania pia zinafurahia kwa kujipatia umaarufu miongo mwa watalii wa Kipoland: Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro. Kwa taarifa zaidi juu ya uchumi wa Tanzania, tunakushauri usome Muongozo wa Uchumi wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Ushirikiano wa Kiutamaduni
Ushirikiano wa Kiutamaduni kati ya Poland na Tanzania unatokea Zaidi kupitia vituo vya moja kwa moja kwa sababu ya mtandao mdogo wa mashirika ya kiutamaduni ya Kipoland katika Afrika. Ingawa, Ubalozi wa Poland wa Dar es Salaam unasaidia kuendeleza ushirikiano wa kiutamaduni kupitia miradi inayotekelezwa Tanzania. Matukio ya kiutamaduni kama vile maonyesho na matamasha yanaanzishwa kwa mpangilio. Kwa mfano, katika mwaka 2018, mfululizo wa masomo yakitolewa na Dr. Eugeniusz Rzewuski kuhusiana na historia ya Poland na Mahusiano ya Poland-Tanzania uliandaliwa Tanzania, pamoja na uonyeshwaji wa filamu ya "Jack Strong", maonyesho ya "Fathers of Independence" na vile vile tamasha la Polish jazz pianists - Piotr Orzechowski, na mwaka 2019 - Sławomir Jaskułke. Pia kulikuwa na ziara mbiliza kimasomo kuenda Poland kwa Waandishi wa Kitanzania kutoka katika magazeti yanayoongoza ya kibinafsi na Kimkoa. Kipendele kilichozoeleka cha kihistoria na kiutamaduni ni makaburi ya Wapoland waliohama wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Necropolies iliyoko Tengeru, Bigwa, Ifunda, Kidugala, Kondoa na wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam. Watu hawa – Raia ambao walilisaidia jeshi lililoundwa na General Władysław Anders – lilifika kwenye Tanganyika ya kipindi hicho kama sehemu ya makazi ambayo ilipangwa na Uingereza katika miliki yake. Wengi wao walihamia Uingereza, Marekani, Kanada na Australia katika kuelekea miaka ya 1940 na 1950, lakini wale waliokufa kwa sababu za magonjwa, ajali au kuamua kubaki Tanzania, walizikwa katika makaburi haya. Ubalozi wa Poland Dar es Salaam umekuwa ukiendeleza kumbukumbu hizi tangu ulipofunguliwa, kuyatunza na kuyafanyia matengenezo.
Ushirikiano katika Sayansi
Mnamo mei 15, 1965 Poland ilisaini Tanzania makubaliano ya ushirikiano wa sayansi na teknolojia. Sasa hivi ushirikiano katika eneo hili unatekelezwa tu kupitia the Ignacy Łukasiewicz Scholarship Programme. Ushirikiano wa kisayansi ni wa kibinafsi na ni matokeo ya vyuo vikuu vya kiserikali na binafsi vya Poland. Aprili 2018, Chuo kikuu cha Maria Curie-Skłodowska kilianzisha mawasiliano na vyuo vikuu vya Tanzania. Wakati huu kinashirikiana na vyuo vingine, chuo kikuu cha Jordan’s University College cha Morogoro.Segerea nje ya Dar es Salaam, kuna kituo cha elimu ambacho kimepewa jina la Saint Maximilian Kolbe kinachoongozwa na Father Franciscan kutoka Poland. Mwaka 2017 msaada wa kifedha wa Poland ulielekezwa kwa wengine wao, kwa ajiri ya ujenzi wa vituo vya elimu ya ufundi na mwaka 2018 kwa utanuzi wa chekechea.
Utambuzi wa sifa za kitaaluma
Nyaraka za uthibitisho wa elimu zinatambuliwa kwa kanuni za ujumla. Poland naTanzania hazikusaini makubaliano yoyote juu ya hili. Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea:
the Ministry of Science and Higher Education
Tanzania Commison for Universities (TCU)