Balozi Buzalski alishiriki katika ziara ya Waziri Tax nchini Poland
21.10.2022
Mnamo Oktoba 17-19, 2022, Balozi Krzysztof Buzalski alishiriki katika mikutano ya Waziri wa Mambo ya Nje Zbigniew Rau na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Stergomena Tax na katika mikutano ya SGGW na PAIH na kampuni za Poland zinazopenda kushirikiana na Tanzania.
Katika mkutano huo, mawaziri hao walifanya mapitio ya kina ya mahusiano baina ya nchi hizo, wakizingatia zaidi miradi inayotekelezwa nchini Tanzania na makampuni ya Poland chini ya mkopo wa serikali. Maeneo mengine yanayotarajiwa ya ushirikiano yalijadiliwa, kama vile usimamizi wa maji na kuweka huduma za mijini kuwa za kidigitali. Mazungumzo hayo pia yalilenga katika ushirikiano wa kimaendeleo – nyanja ambayo Tanzania ni miongoni mwa washirika wa kipaumbele wa Poland. Matarajio ya maendeleo ya usafiri wa anga na upanuzi zaidi wa kubadilishana wanafunzi pia yalijadiliwa. Waziri Rau na Waziri Tax pia walishirikishana tathmini zao za matokeo ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Waziri Tax pia alitembelea Kituo cha Maji cha Chuo Kikuu cha Warsaw cha Sayansi ya Maisha, na kushiriki katika mkutano na makampuni katika makao makuu ya Shirika la Uwekezaji na Biashara la Poland na mkutano na wawakilishi wa Cluster ya Usalama wa Mtandao katika makao makuu ya Asseco Poland S.A.