Habari
-
13.12.2024Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Jakub Wiśniewski nchini TanzaniaZiara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland Jakub Wiśniewski nchini Tanzania tarehe 11-12 Desemba 2024, iliruhusu kubadilishana mawazo na wawakilishi wa mamlaka za Tanzania kuhusu uwezekano wa ushirikiano wa maendeleo, uwekezaji na biashara kati ya Poland na Tanzania. Pia ilikuwa ni fursa ya kukutana na wanufaika wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa jijini Dar es Salaam kwa mfuko ya Polish Aid.
-
10.12.2024Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa UlayaMazungumzo ya kwanza ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya chini ya Mkataba wa Samoa yalifanyika tarehe 10 Desemba 2024 jijini Dar es Salaam.
-
02.12.2024Tunaendelea na juhudi za kulinda mazingira na kukuza ujasiriamali katika Bonde la Kilombero na Milima ya Udzungwa.Konseli wa Jamhuri ya Poland, Wojciech Łysak, alitembelea eneo la mradi wa maendeleo unaoendeshwa na shirika la Southern Tanzania Elephant Program (STEP) kwa msaada wa Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam. Malengo ya msingi ya mradi ni kukuza kuishi pamoja kwa amani kati ya binadamu na tembo katika bonde la Kilombero na kuimarisha maisha ya wajasiriamali wa ndani. Mpango huo unafadhiliwa na mfuko wa Polish Aid.
-
02.12.2024“Feast of Fire” kwenye tamasha la filamu la “ZIFF Goes Mainland”Kama sehemu ya toleo la 2024 la Tamasha la Filamu la "ZIFF Goes Mainland", lililofanyika kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 21, 2024, filamu kutoka nchi za Afrika na mataifa kumi ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na Poland na Ukraine, ziliwasilishwa.
-
29.11.2024Siku ya Uhuru wa Poland nchini TanzaniaNovemba 8, ubalozi wetu ulikuwa na sherehe ya kuadhimisha miaka 106 ya Poland kupata uhuru wake. Tuliwakaribisha Wapolandi waishio Tanzania na watanzania waliohitimu vyuo mbalimabali Poland kujumuika nasi katika maadhimisho hayo.
-
29.11.2024Tunaunga mkono juhudi za kurudisha msitu wa hifadhil wa MagomberaKonseli wa Jamhuri ya Poland Wojciech Łysak alitembelea maeneo yenye miradi ya maendeleo yanayoungwa mkono na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa mfuko wa Polish Aid katika msitu wa Magombera
-
01.11.2024Kwenye Sikukuu ya Watakatifu Wote Tulitembelea Makaburi ya Wapoland Tanzania.Kuadhimisha Sikukuu ya Watakatifu Wote, kaimu balozi Katarzyna Sobiecka na mkuu wa idara ya utawala na uhasibu, Bw. Edgar Klusa waliweka maua kwenye makaburi ya ndugu Makaburini Kinondoni, Dar es Salaam. Konseli wa Jamhuri ya Poland, Wojciech Łysak alitembelea makaburi ya wapolish yaliyopo Ifunda, karibu na Iringa, na Konseli msaidizi Krystyna Fatyga alitembelea makaburi ya Wapoland yaliyopo Bigwa, karibu na Morogoro.
-
22.08.2024Tunaendelea kusaidia jamii ya albino nchini TanzaniaMatatizo ya kiafya, ukosefu wa elimu stahiki na ujuzi wa kitaalamu unaowakwamisha kupata ajira, pamoja na kutengwa na jamii, bado ni changamoto kubwa zinazowakabili watu wenye ualbino nchini Tanzania. Mradi wa ‘Mustakabali bora kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania’ unaofadhiliwa na Polish Aid kimsingi unalenga kuwapa watu hao nafasi sawa za kuishi maisha bora.
-
07.08.2024Ufunguzi wa Kongamano la Kiesperanto la Dunia nchini Tanzania kwa Ushiriki wa Mwakilishi wa Ubalozi.Kongamano la Dunia la Kiesperanto lililofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 3-10 mwaka huu, limewakutanisha zaidi ya wazungumzaji mia saba sabini wa lugha ya Esperanto kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Ufunguzi wa tukio hili la kipekee, lenye lengo la kukuza uelewa wa kimataifa na kubadilishana utamaduni, pia ulihudhuriwa na mwakilishi wa ubalozi wetu - Naibu Konseli Krystyna Fatyga.
-
06.08.2024Tulitembelea Makaburi ya Poland huko TengeruNaibu Konseli wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Krystyna Fatyga, alipotembelea makaburi ya wakimbizi wa Poland yaliyopo Tengeru pamoja na washiriki wa Kongamano la Dunia la Kiesperanto, lililofanyika mwaka huu jijini Arusha.