Balozi Buzalski atembelea miradi ya maendeleo katika Bonde la Kilombero
11.04.2023
Msaada wa Ubalozi na Msaada wa Poland (yaani Polish Aid) kwenye sehemu ya kuishi kwa amani baina ya watu na tembo, maendeleo endelevu ya jumuiya za mitaa, pamoja na ujenzi wa huduma za kisasa ya zimamoto, zilikuwa ni mada ya mazungumzo kati ya Balozi Krzysztof Buzalski na timu ya walinzi wa hifadhi ya taifa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali katika Bonde la Kilombero.
Katika kipindi cha Machi na Aprili mwaka huu, Balozi Krzysztof Buzalski alitembelea Bonde la Kilombero, ambapo, kupitia sehemu ya ruzuku ndogo ya Msaada wa Poland (yaani Polish Aid), Ubalozi umekuwa ikisaidia shughuli za shirika lisilo la kiserikali la STEP katika ulinzi wa bioanuwai ya Tanzania na hali ya amani baina ya watu na wanyama pori.
Lengo la Msaada wa Poland (yaani Polish Aid) ni kuhakikisha urejeshwaji wa idadi ya tembo ulimwenguni sambamba na uboreshaji wa usalama, ustawi na riziki ya jumuiya za mitaa. Balozi Buzalski alikutana na wawakilishi wa ushirika wa mikopo midogo kutoka kijiji cha Msolwa katika Bonde la Kilombero, ambao walimuelezea kuhusu fursa za kimaendeleo walizozipata kutokana na mradi ambao Ubalozi unatekeleza pamoja na shirika la STEP.
Balozi pia alishiriki katika kampeni ya kupanda miti katika ushoroba ya tembo kwenye Bonde la Kilombero na shirika za STEP na Reforest Africa zinazosaidia kutengeneza njia ya kwanza ya wanyama pori nchini Tanzania itakayoonganisha hifadhi za taifa.