Kwenye Sikukuu ya Watakatifu Wote Tulitembelea Makaburi ya Wapoland Tanzania.
01.11.2024
Kuadhimisha Sikukuu ya Watakatifu Wote, kaimu balozi Katarzyna Sobiecka na mkuu wa idara ya utawala na uhasibu, Bw. Edgar Klusa waliweka maua kwenye makaburi ya ndugu Makaburini Kinondoni, Dar es Salaam. Konseli wa Jamhuri ya Poland, Wojciech Łysak alitembelea makaburi ya wapolish yaliyopo Ifunda, karibu na Iringa, na Konseli msaidizi Krystyna Fatyga alitembelea makaburi ya Wapoland yaliyopo Bigwa, karibu na Morogoro.
Ubalozi wa Poland Dar es salaam untunza maeneo matano yaliyo na makaburi ya Wapoland, pamoja na idadi kubwa ya makaburi ya Wapoland jijini Dar es Salaam. Zaidi ya ndugu zetu mia mbili wamezikwa kwenye haya maeneo. Wengi wao ni raia walioambatana na jeshi la Generali W. Andres katika safari yake kutoka Muungano wa Kisovieti kwenda Irani na Palestina. Askari wa jeshi la usalama la kipolish waliyo kuwa USSR walikwenda vitani, wakati raia walisafirishwa na kuweka makazi kwenye makoloni ya waingereza, ikiwemo Tanganyika (Tanzania). Hapa, waliweka makazi ya Wapoland kubwa zaidi kule Tengeru (kama wakazi 5000), karibu na Arusha mjini. Miaka ya 1940 na 1950, baadhi yao walihamia Uingereza, Marekani, Kanada, Australia na nchi zingine, na wengine kubaki Tanzania.
Kati ya mwaka 2018 na 2021, kwa ushirikiano kati ya vituo mbalimbali na Ubalozi wa Poland, Dar es salaam, matengenezo ya makaburi yote ya Wapoland kwenye maziara yote Tanzania yalifanyika kwa mafanikio. Maziara yote yanafanyiwa marekebisho mara kwa mara inapohitajika, kusafishwa na kutembelewa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Poland, Dar es salaam. Mapema mwaka huu Agosti, Konseli msaidizi Krystyna Fatyga, akiambatamna na washiriki Wapoland kwenye World Esperanto Congress, walitembelea makaburi ya Tengeru.