Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Maadhimisho ya miaka 231 tangu kupitishwa kwa Katiba ya Tarehe 3 Mei na siku ya Wapoland waishio nchini Tanzania

07.05.2022

Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani za Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Me na kusoma barua kutoka kwa Waziri SzynkowskivelSęk yenye pia ujumbe wa kuwatakia kila la kheri wakazi wote wenye asili ya Kipoland waishio nchini.

3_maja_2022 Dar_0

Katika sherehe hizo, maonesho ya kuadhimisha miaka 80 ya kuwasili kwa wakimbizi wa Kipolishi nchini Tanganyika yaliwasilishwa. Walipata hifadhi barani Afrika baada ya kutoroka mnamo 1942 kutokana na uchokozi uliotokana na  Muungano wa Soviet. Maonyesho hayo yalitayarishwa kwa ajili ya Ubalozi na watayarishaji walikuwa ni Kituo cha Nyaraka za Uhamishwaji, Ufukuzwaji na Uhamisho cha Chuo Kikuu cha Pedagogical huko Krakow. Zaidi ya hayo, pia tulionyesha maonyesho ya picha kuhusu msaada wa Poland kwa Ukraine baada ya uvamizi wa Kirusi.

Balozi Buzalski pia aliwasilisha salamu zake mwenyewe kwa Wapoland waliokusanyika na wahitimu wa Kitanzania wa vyuo vikuu vya Poland na kuwahimiza kudumisha mawasiliano endelevu na Ubalozi.

Mkutano huo pia ulikuwa ni fursa ya kuonja chakula cha kitamaduni cha Kipolandi, ambacho tulijitayarishia wenyewe, kwa sauti za muziki wa Kipolandi na wa kimataifa.

Picha (9)

{"register":{"columns":[]}}