Maadhimisho ya miaka 232 tangu kupitishwa kwa Katiba ya Tarehe 3 Mei nchini Tanzania
05.05.2023
Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Mei na kufafanua zaidi kuhusu historia ya Poland na mafanikio ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.
Mada ya hotuba hiyo ilikuwa ni muhtasari wa mahusiano mazuri kati ya Poland na Tanzania, pamoja na utekelezaji wa miradi ya pamoja. Kipaumbele ilipewa maada ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na msaada uliotolewa na Poland na Wapoland kwa nchi hiyo na kwa watu wake.
Hafla hiyo ilyokuwa na chakula cha Kipolishi iliwakusanya wageni wengi, ikiwa pamoja na viongozi wa serikali ya Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, wanadiplomasia, Wapoland na wahitimu wa vyuo vikuu vya Poland nchini Tanzania. Balozi Buzalski alitoa hotuba, kwa lugha ya Kipolishi, ya Kiingereza na ya Kiswahili, ambayo ilipokelewa vizuri na kuthaminiwa na wageni waliohudhuria.
Maadhimisho pia yalitoa fursa ya kutazama maonyesho ya "POLSKA" yaani „POLAND” na kusikiliza muziki wa Kipolish na tamasha la muziki la saksofoni.
Hafla hii ilikuwa sehemu ya Siku za Urithi wa Poland, ambazo hivi karibuni zimekuwa zikiadhimishwa mwezi Mei ulimwenguni kote.