Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Mabadiliko ya ada ya Viza - Viza ya aina D (Viza ya taifa) na C (Viza ya Schengen)

31.05.2024

preview_announcement_new

Ofisi ya Konsula (kitengo cha Viza) ya Ubalozi wa Jamhuri ya Poland, Dar es Salaam inapenda kuwataarifu kuwa ada ya kupokea na usindikaji wa maombi ya Visa ya taifa (aina ya D) na ada ya kupokea na usindikaji wa maombi ya kuangaliwa upya ya Viza ya taifa yatafanyiwa marekebisho kuanzia Juni 1, 2024. Kuanzia Juni 1 mwaka huu, ada itakuwa dola (USD) 150, mia moja hamsini.

Pia kuanzia Juni 11, 2024, ada ya kupokea na usindikaji wa maombi ya Viza ya Schengen (aina ya C) itakuwa dola (USD) 100, mia moja. Kwa waombaji wa umri miaka 6 hadi 12 ada itakuwa dola (USD) 50, hamsini. Mabadiliko haya yanatokana na ukaguzi wa mara kwa mara wa ada na Tume ya Nichi za Ulaya.

Ada ya kuangaliwa upya, kupokea na usindikaji wa maombi ya Viza ya aina ya Schengen (aina ya C) haijabadilika, ni dola (USD) 89, themanini na tisa.

 

{"register":{"columns":[]}}