Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Makaburi mengine ya Poland nchini Tanzania - huko Kidugala - yamekarabatiwa

28.12.2021

Shukrania kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kituo cha nyaraka,ufukuzwaji na uhamisho wa Chuo Kikuu cha Pedagogical huko Cracow,wakfu wa PU “pro Univesitatis” na Wizara ya Utamaduni na Urithi wa kitaifa, makaburi mengine ya Poland nchini Tanzania yamekaratiwa.

Kidugala 2021_0

Necropolis huko Kidugala ni mahali pa mazishi ya Poles ambao baada ya kuzuka vita ya pili ya dunia, walifukuwa ndani ya USSR, na kama matokeo ya makubalianao ya Sikorski-Majski waliweza kuondoka mahali pa uhamisho na mnamo 1942 walipata kimbilio katika makazi barani Afrika. Moja ya makazi sita kama hayo ya wapoland katika Tanzania leo, zamani Tanganyika, yalikuwa ni yale ya Kidugaka. Mnamo Desemba 1944, yalikaliwa na karibu raia 800 wa kipolishi na mnamo 1954-kama watu 900. Eneo hilo mbali na nyumba za makazi lilikuwa na kilabu ya skauti, nyumb ya kuoga, shule ya msingi na shule ya sekondari ya bweni, hospitali nyumba ya kipolishi na kanisa la wamishionari. Pia lilijumuisha sehemu kadhaa za kazi kama vile duka la useremala, ghushi au chumba cha kushona. Makaburi pia yalianzishwa ndani ya eneo hilo na mnamo 1944 lilizungushiwa ukuta.

Kazi za matengenezo na ukarabati katika necropolis hii ambayo ilidumu kwa wiki tatu zilisimamiwa na Pro. Hubert Chudzio kutoka Taasisi ya historia na hifadhi ya Chuo kikuu cha Pedagogical, mkurugrnzi wa kituo cha nyaraka za uhamisho, ufukuzwaji na makizi mapya ya Chuo kikuu cha Pedagogical huko Cracow. Zilifadhiliwa na Wizara ya utamaduni na Urithi wa kitaifa wa Poland kama sehemu ya mpango wa makumbusho ya kitaifa nje ya nchi 2021. Shukrani kwa fedha kutoka wizara ya Mambo ya nje ya Jamhuri ya Poland iliyolenga kusaidia diaspora ya Poland nje ya nchi, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam ulifadhili uchapishaji na uwekaji wa mabango mapya ya taarifa kwenye makaburi na kusaidia timu ya Prof. Chudzio kwa mpangilio.

Picha (7)

{"register":{"columns":[]}}