Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Masada wa Kipolandi nchini Tanzania unalenga kuboresha afya ya wanawake

07.11.2022

Shukrani kwa fedha za Msaada wa Kipolandi na msaada wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Kliniki ya Ushauri ya Upasuaji ya Pendo katika mji wa Mtwara nchini Tanzania imekamilisha mradi wa miezi kadhaa uliotekelezwa mwaka 2022, unaolenga kuandaa programu ya utambuzi wa awali wa saratani ya matiti katika mkoa huo.

Mtwara 2022_1

Miongoni mwa magonjwa yote ya saratani, saratani ya matiti ndiyo inayoongoza kwa vifo vya wanawake. Nchini Tanzania, wagonjwa wengi walio na aina hii ya saratani huripoti kwa daktari wakiwa wamechelewa kupata matibabu madhubuti. Hali hii inaweza kuboreshwa kwa kueneza maarifa juu ya saratani ya matiti kati ya wahudumu wa afya na jamii, na kuanzisha mfumo wa uchunguzi kwa jamii ya wanawake ili kuruhusu utambuzi wa mapema wa ugonjwa huu.

Kwa hiyo lengo la mradi huo lilikuwa kupunguza idadi ya wagonjwa wa saratani ya matiti waliosahaulika, kuwezesha wanawake kupata matibabu mapema, na hivyo kupunguza vifo vya wanawake katika mkoa wa Mtwara. Ilijumuisha kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa karibu vituo vyote vikubwa vya kutolea huduma za afya katika eneo la Mtwara, akiwemo Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula, Mkuu wa kituo cha afya Likombe, Mganga Mkuu wa Wilaya na Wakuu wa zahanati 18 za mitaa. Wote wamejitolea kuteua wafanyakazi wanaohusika na kuendeleza kampeni ya mafunzo miongoni mwa wafanyakazi wa matibabu ndani ya vituo vyao husika na wamepokea zana muhimu za mafunzo. Mafunzo mengine pia yalifanyika kwa zaidi ya wanawake 100 wanaofanya kazi katika kiwanda cha saruji cha ndani ambao pia wataweza kushirikisha maarifa waliyopata kwa marafiki zao. Zaidi ya hayo, kampeni ya habari kupitia redio ya ndani iliwezesha kusambaza maarifa muhimu kuhusu kinga na uchunguzi wa kimsingi wa matiti kwa maelfu ya wasikilizaji. Kutokana na hatua hiyo tayari wanawake ambao wamekuwa wakishuku kuwa na vidonda wameanza kutembelea zahanati ya Pendo ili kufanyiwa uchunguzi na ikibidi kufanyiwa upasuaji. Mbali na mafunzo na kampeni ya habari, mradi ulifanikisha kuipa kliniki ya Pendo vifaa vya matibabu na vifaa vingine muhimu.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka, alipotembelea zahanati ya Pendo na mkurugenzi wake, daktari wa upasuaji kutoka Poland Ryszard Jankiewicz, ambaye alisimamia mradi huo unaofadhiliwa na ruzuku ndogo. Ziara hiyo imeuruhusu Ubalozi wetu sio tu kufahamu matokeo ya mradi huo papo hapo, lakini pia kupata ufahamu wa kina zaidi juu ya hali ya kazi ya wahudumu wa afya wa eneo hilo na mahitaji zaidi ya mkoa katika uwanja wa afya, ambayo ni moja ya maeneo muhimu ya maslahi kwa ushirikiano wa maendeleo wa Poland nchini Tanzania.

Picha (4)

{"register":{"columns":[]}}