Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Mfuko wa misaada wa Poland kuendelea kuisaidia Tanzania katika mapambano yake dhidi ya Kifua Kikuu

05.12.2021

Ulinzi wa afya ni mojawapo ya vipaumbele vya ushirikiano wa maendeleo wa Poland na nchi za Afrika. Ndio maana mwaka huu tunaendelea kufadhili mradi wa shirika la APOPO unaotekelezwa nchini Tanzania, unaojumuisha kugundua ugonjwa wa kifua kikuu kwa msaada wa panya wakubwa wa kusini.

Apopo_Dar 2021_5

Kifua kikuu ni mojawapo ya visababishi kumi vya kawaida vya vifo nchini Tanzania. Pia husababisha matatizo mengine kama vile kutengwa kijamii na kiuchumi (hisia ya aibu na woga inayohusishwa na utambuzi, kukubali ugonjwa na matibabu yanayohusiana nao, miongoni mwa mengine, hatari ya kupoteza kazi, na ikiwa kazi hiyo ndiyo chanzo pekee cha mapato kwa familia nzima.)

Shirika la APOPO limekuwa likibuni mbinu ya kuwafunza panya wakubwa wa kusini walio na uwezo mkubwa wa kunusa na akili, ambao wana uwezo wa kutambua kwa usahihi na haraka uwepo wa kifua kikuu kwenye sampuli za makohozi zinazokusanywa kutoka kwa wagonjwa katika kliniki zinazoshirikiana na shirika hili. Zaidi ya hayo, harufu ya panya hao makini au hata makini zaidi kuliko hadubini iliyotumiwa ndani ya ‘smear ya sputum’. Matumizi ya panya katika eneo hili pia ni nafuu zaidi kuliko matumizi ya vipimo vya jadi vya maabara.

Mnamo mwaka wa 2019, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, pamoja na APOPO, ulitekeleza mradi wa kupanua programu ya kugundua kifua kikuu nchini Tanzania kwa njia za panya na kuipatia APOPO chanzo cha nishati ya kiikolojia na cha uhakika. Kutokana na mradi huo, zahanati nyingine za mikoa ya Dodoma na Morogoro zilijumuishwa katika mpango wa utambuzi wa kifua kikuu. Kwa sasa, Mfuko wa msaada wa Poland unajihusisha na mradi unaolenga kuharakisha ugunduzi wa ugonjwa wa kifua kikuu katika mazingira yenye rasilimali chache jijini Dar es salaam kwa kuongeza kiwango cha ugunduzi wa wagonjwa wa kifua kikuu na kufanya huduma za afya zinazohusika na ugonjwa huu kupatikana kwa wagonjwa zaidi. Shukrani kwa msaada wetu, kliniki nyingine tatu za Dar es Salaam tayari zinashiriki katika mpango huu.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Poland Dar es Salaam, Katarzyna Sobiecka hivi karibuni ametembelea maabara ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa panya inayoendeshwa na shirika la APOPO, Ambapo alipata fulsa ya kujionea namna ya ufanyaji kazi na panya hao ulivyo kivitendo. Katika dakika chache tu, mnyama huyo aliweza kutambua sampuli zilizotiliwa wasi wasi kati ya sampuli 50 zilizoweka katika vipimo. Hii ni kazi ambayo vifaa vya kawaida vya maabara vingeweza kutumia siku kadhaa ili kuweza kubaini.

 

Picha (7)

{"register":{"columns":[]}}