Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Msaada wa Kipoland unasaidia kuboresha elimu, usafi na mazingira ya usafi wa jamii katika eneo la Kiabakari

06.04.2022

Upande wa Kaskazini – Magharibi mwa Tanzania – huko Kiabakari – miradi miwili ya maendeleo iliyofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland katika mashindano ya Polish Development Aid ya 2021 na kutekelezwa na Kiabakari Foundation pamoja na Parokia ya Kikatoliki ya Kiabakari imezinduliwa.

Kiabakari_04 2022_1

Kutokana na mradi wa Shule yangu, Nyumba yangu (My school, My home) bweni la ghorofa mbili la kisasa lililopo jirani kabisa na shule ya msingi Kiabakari limejengwa na sasa lipo tayari kuhudumia wasichana 200 kutoka mkoa wa Mara Tanzania, ambao vinginevyo wasingeweza kuhudhuria shule  na hivyo kunyimwa nafasi ya elimu. Litawasaidia pia watoto wanaoteseka katika maisha yao ya kila siku kutokana na makazi duni, hali ya usafi na lishe, pamoja na watoto kutoka familia zilizo katika hatari ya ukatili ambao hawana fursa ya kusoma nyumbani. Kama sehemu ya mradi huo, tathmini ya ziada ya kinga ilifanywa kwa wanafunzi 300 wa shule ya msingi, ambayo iliruhusu kutathmini afya za watoto , na pia kuchukua hatua zinazofuata ili kuhakikisha utambuzi wowote zaidi na matibabu sahihi. Zaidi ya hayo,mfululizo wa mafunzo ndani ya wiki ya afya na usafi ulifanyika, na zaidi ya hayo watoto walipokea vifurushi vya usafi.

Mradi wa pili, unaoitwa Mvua na Jua – Lengo Moja (Rain na Sun- One Purpose), unaolenga kuhakikisha usalama wa nishati na uhuru wa kituo cha afya cha Kiabakari na Kuimarisha usalama wa usafi na usalama dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa jamii . Mbali na ujenzi na ufungaji wa hatua ya usafi, mifumo miwili mikubwa ya photovoltaic imewekwa kwenye vituo viwili vya afya vya eneo hilo. Mifumo hiyo inaruhusu kubadili kati ya matumizi ya nishati ya jua/umeme na kufaidika na nishati ya jua hata kwa shughuli za upasuaji. Kama sehemu ya mradi huo, iliandaliwa huduma ya mafunzo juu ya usafi na usalama, pia kuhusiana na janga la Corona.

Sherehe za ufunguzi wa miradi hiyo zilihuzudhuriwa na wanajamii ambao miongoni mwao ni walimu, watoto na wazazi wao, wawakilishi wa serikali na mapadri wa Tanzania akiwemo Askofu Michael George Mabuga Msonganzila, mgeni wa heshima – Jenerali Meja Michael Joseph Isamuhyo, mratibu wa hafla hiyo na mshirika wa mradi Paroko wa Parokia ya Kiabakari Wojciech Koscielniak, rais wa Kiabakari Foundation  BożenaKoczur na mwakilishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam Katarzyna Sobiecka.

Picha (5)

{"register":{"columns":[]}}