Msaada wa Poland kusaidia uwezeshwaji wa muingiliano wa maisha ya binadamu na tembo katika Bonde la Kilombero nchini Tanzania
09.10.2021
Katika ratiba ya utendaji kazi wa msaada wa Kipoland, Ubalozi wa Jamuhuri ya Poland Dar es Salaam unawezesha hatua za shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kazi kwa manufaa ya kuboresha muingiliano wa kimaisha wa watu na tembo katika Bonde la Kilombero. Lengo ni kutafuta ufumbuzi katika eneo la mwingiliano wa kimaisha baina ya wanyama na jamii ya wenyeji, kwa kuzingatia tatizo linalosababishwa na upanuzi wa makazi ya watu na kilimo kwenye maeneo ambayo wanyama hao wapo, kwa mfano kando kando ya mipaka ya maeneo hifadhi.
Hili linafanyika kwa upande mmoja, kwa kuwaelimisha na kukuza uelewa wa watoto (progarmu za elimu za shule) na watu wazima (mfano. Uonyeshaji wa filamu usiku) zikihusisha tabia za tembo pamoja na kanuni za kiusalama dhidi ya wanyama hawa waliopo, umuhimu wa uhifadhi wa viumbe hai na uunganiko wa kiikolojia, na vilevile kupitia mfumo wa kuwatembelea wanafunzi wenyeji katika maeneo ya hifadhi, na kwa upande mwingine kuboresha njia za kupunguza matokeo ya migogoro baina ya binadamu na tembo.
Mpaka sasa, njia ya msingi ya kulinda eneo la mashamba dhidi ya tembo imekuwa ni kutengeneza uzio wa mizinga ya nyuki, kwa sababu ya ufanisi wake wa kiwango cha juu na upatikanaji wa sehemu nzuri kando kando ya mashamba, vilevile imeongeza thamani kwa wafugaji wa nyuki (faida iliyopatikana kwa kuuza asali). Kama sehemu ya mradi, vibanda maalum pia vimejengwa ili kuwezesha uhifadhi wa mizinga ya nyuki kabla ya kusafirishwa kwenda kwenye eneo husika la uzio.
Ingawa, kwa sababu ya sababu zilizo nje kama vile mafuriko ya msimu katika baadhi ya maeneo ya Kilombero, zinapelekea kuto kuwezekana kuweka mizinga katika maeneo haya, njia nyingine mbili za kiubunifu ziko katika majaribio wakati huu: kutengeneza uzio wa taa za kutumia nguvu ya jua (strobe lamp) na pia uzio uliotengenezwa na vyombo vyenye harufu iliyotengenezwa kiasili, viungo vichachu ikiwa ni pamoja na pilipili na vitunguu swaumu.
Mradi pia unawezesha uzalishaji wa dawa za harufu zenyewe, kwa kuwa zinatakiwa kuwekwa nyingine mpya kila mwezi. Hawa ni wakulima wenyeji ambao wanahusika katika mchakato wa uzalishaji, Ufanisi wa aina hii ya uzio – ambao unakaguliwa shukrani kwa waangalizi wenyeji na utegaji wa picha – kuthibitisha kuwa chini kuliko ule wa uzio wa mizinga ya nyuki au uzio wa taa, lakini gharama za ujenzi wake ziko chini pia.
Mapema wiki hii, wakati wa usimamizi wa utekelezwaji wa mradi kwa hatua yaani kutoka katika Mfuko wa msaada wa Poland, mwakilishi wa Ubalozi wa Jamuhri ya Poland uliopo Dar es Salamaa Katarzyna Sobiecka, alipata fulsa sio tu ya kutembelea uzio uliokwisha kujengwa na kuangalia mchakato wa uzalishaji wa madawa ya harufu, lakini pia kukutana na wakulima wenyeji na wafugaji wa nyuki ambao walithibitisha manufaa ambayo jamii imeyapata kutoka kwenye mradi, kwa kulinganisha na mazao machache waliyoyapoteza kutokana na uvamizi wa tembo katika mashamba yao.
Pia alihudhuria mkutano wa wiki wa moja ya kijiji kati ya vijiji sita wa vyama vya akiba na mikopo (VSLAs) vilivyoanzishwa ndani ya mradi. Ni hatua ya elimu ya kifedha ambayo imeleta manufaa yanayoonekana kwa wakulima kwa kuwawezesha, kwa mfano, kuweka riba ndogo kwa mikopo ya kifedha ambayo inawawezesha kujizuia kuuza mazao yao mpaka wakati yanapoongezeka thamani.
Mradi unaendeshwa katika ufahamu wa malengo ya maendeleo endelevu, ikijumuisha: lengo la 1: tokomeza umasikini, lengo la 2: maliza njaa. lengo la 5: usawa wa kijinsia, lengo la 15: maisha na ardhi. Inakamilisha mwendelezo wa hatua ya kufanya kazi na jamii katika bonde la Kilombero kuinua upya njia ya maisha ya wanyama poli inayounganisha milima ya Udzungwa na Mbuga ya Taifa ya Nyerere. Njia imeundwa ili kuendeleza hatua ya mwingiliano miongoni mwa jamii ya tembo wa Kusini ya Tanzania.