Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Onesho la filamu ya "The coldest Game" ufunguzi wa maonyesho ya "John Paul wa pili - Papa wa mdahalo"

25.09.2020

Mnamo Septemba 25, 2020 Ubalozi wa Jamuhuri ya Poland Dar es Salaam iliandaa onyesho la filamu ya "The coldest Game" kwenye ukumbi Alliance Francaise  na ufunguzi wa maonyesho ya "John Paul wa pili - Papa wa Mdahalo".

The Coldest Game

Filamu iliongozwa na Lukas Kosmicki, ilipokea tuzo kadhaa za kimataifa mwaka 2019 na tuzo maalum ya tamasha la 44 la filamu za Kipoland Gdynia. Maonyesho yaliandaliwa katika hafla ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa John Paul wa pili ambayo inasherekewa mwaka huu.

Tukio hili lilihudhuriwa na wafanyakazi wa Ubalozi akiwemo Balozi Krzysztof Buzalski Balozi wa kimitume wa katoliki Tanzania, Abp Mereki Solczynski, wawakilishi wa polisi wa kidiplomasia, vilevile na jamii ya watu wa Poland na marafiki zetu wa Tanzania.

Katika hotuba yake, Balozi Krzysztof Buzalski alirejea kwenye kipindi cha Vita Baridi kilichowasilishwa kwenye filamu na kurejea kwenye nguvu kubwa muhimu zilizoukomesha ukomunisti Poland: muungano wa kibiashara "Mshikamano" (sasa ikiwa ni kumbukumbu ya kutimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake) na Papa John Paul wa pili katika kipindi chake cha upapa (sasa ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwake).

Picha (5)

{"register":{"columns":[]}}