Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Shukrani kwa msaada wa Wapoland, Tunaandaa jengo jipya la Chekechea- ‘Holy Family Day Care’ huko Segerea

22.10.2021

Fenicha mpya za shule, magodoro pamoja na jiko, vifaa vya kufulia na uwanja wa michezo vitahudumia watoto wadogo kutoka Segerea hivi karibuni, Wilaya ya Dar es Salaam, pamoja na wafanyakazi wa shule wanaofanya kazi katika shule ya chekechea. Ununuzi wa vitu vya msaada wa Poland utawawezesha Masista Wamisionari wa Familia Takatifu kufungua hivi karibuni jengo jipya la Chekechea-Holy Family Day Care.

Segerea 2021_1

Eneo la mradi lilitembelewa na mwakilishi wa ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam Katarzyna Sobiecka, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji. Alipata fursa ya kuzungumza na mmisionari wa Kipolandi anayesimamia mradi unaofadhiliwa ndani ya ushirikiano wa maendeleo wa Poland, na pia kukutana na wanafunzi wadogo kabisa wa kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian cha Dar es Salaam na kutembelea shule mpya za Chekechea.

Kadri jiji la Bandari linavyokua kwa kasi, Dar es Salaam inavutia watanzania wengi wanaotafuta kazi, ikiwa ni pamoja na familia zilizopanuka. Shirika la Masista Wamisionari wa Familia Takatifu wakiwemo wamisionari kutoka Poland wanaoshirikiana na Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian cha jijini Dar es Salaam, wanasaidia wazazi wanaofanya kazi kwa kutoa malezi na elimu ya mchana kwa watoto wao wakiwemo walio katika umri wa kwenda shule za awali.

Kwa sababu ya hitaji kubwa la jamii ya eneo hilo la msaada kama huo, hasa katika familia ambapo wazazi wote wanafanya kazi, Kwa sasa kutaniko linajitayarisha kufungua chekechea katika jengo jipya lililojengwa. Madhumuni ya mradi unaotekelezwa katika mfumo wa msaada wa Kipoland ni kuandaa fenicha na vifaa muhimu. Walengwa wa mradi huo watakuwa wanafunzi wa shule ya chekechea, walimu na wafanyakazi wasaidizi, na pia kwa njia isiyo ya moja kwa moja- familia zao zote.

Picha (5)

{"register":{"columns":[]}}