Siku ya Uhuru wa Poland nchini Tanzania
29.11.2024
Novemba 8, ubalozi wetu ulikuwa na sherehe ya kuadhimisha miaka 106 ya Poland kupata uhuru wake. Tuliwakaribisha Wapolandi waishio Tanzania na watanzania waliohitimu vyuo mbalimabali Poland kujumuika nasi katika maadhimisho hayo.
Wakati wa maadhimisho, wageni waliweza kuangalia maonyesho ya “Outstanding Polish Women”, maalum kwa wanawake waliojipambanua, ambao mafanikio yao yalikuwa na tija kwenye ustaarabu na maendeleo ya kiutamaduni ya sio tu Poland bali Dunia nzima kwa ujumla, kuchangia maendeleo kwenye nyanja za sayansi, utamaduni, sanaa na siasa.
Katarzyna Sobiecka, mkuu wa misheni, aliwasilisha salamu zake kwa Wapolandi walioudhulia, alitilia mkazo umuhimu wao kwenye uhusiano wa maendeleo kati ya Poland-Tanzania. Alielezea shukrani zake kwa juhudi zao za siku zote, ambazo zimeimarisha mshikamano baina ya nchi hizi mbili na ni msingi wa muhimu katika kujenga taswira chanya ya Poland Tanzania.
Sherehe ilikuwa pia ni fursa muhimu ya kuwaunganisha jamii ya Wapoland wa ndani na kujenga mahusiano mapya. Wageni walikuwa na fursa ya kujaribu vyakula vya kipoland vilivyoandaliwa maalumu kwa siku hii. Sherehe ilisindikizwa na muziki wa kipoland na wa kimataifa, ambapo iliongeza hali nzuri ya mkutano na kuchangia hali nzuri ya mazungumzo na kusherehekea kwa pamoja kwenye sherehe hii muhimu.