Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Tamasha la piano la Jan Krzysztof Broja na Maonyesho ya „Mama, sitaki vita!”

15.03.2023

Tarehe 15 Machi 2023, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ujerumani, uliandaa tamasha la piano lililochezwa na mpiga kinanda mahiri wa Poland, Jan Krzysztof Broja, pamoja na kuwasilisha maonyesho ya Kipoland-Kiukraine yaitwayo "Mama, sitaki vita!", sambamba na maadhimisho ya hivi karibuni ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Koncert_JKBroja 2023_0

Tamasha lilianza kwa hotuba wa Balozi Krzysztof Buzalski aliyemtambulisha mpigaji kinanda na kuwasilisha mlolongo wa tamasha, ambalo lilijumuisha kazi za Frederic Chopin, Karol Szymanowski, Michał Kleofas Ogiński, Johann Sebastian Bach, Ludwig van Beethoven, na Johannes Brahms. Balozi Buzalski aliwahimiza wageni kutazama maonyesho ya "Mama, sitaki vita!" ya michoro ya kisasa ya watoto wa kutota Ukranie. Maonyesho hayo yalionyeshwa sambamba na maadhimisho ya hivi karibuni ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Jan Krzysztof Broja ni mmoja wa wapiga piano bora barani Ulaya, mshiriki wa Shindano la 13 la Chopin mwaka 1995, ambaye ameshinda tuzo nyingi katika mashindano ya piano ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Hanau nchini Ujerumani (1989), Braunschweig nchini Ujerumani (1991), Bucharest nchini Romania (1995), Warsaw (1995), Vilnius nchini Lithuania (1999) na Pasadena / Los Angeles nchini Marekani (2002). Mwaka wa 2009, aliteuliwa kama mpigaji kinanda wa kwanza wa Kipolandi huko Los Angeles kwa tuzo ya juu zaidi ya muziki, Tuzo ya Grammy ya Chuo cha Fonografia cha Amerika.

Pia, msanii huyu anajulikana kwa ushiriki wake katika utayarishaji wa filamu kadhaa muhimu za televisheni na sinema. Kazi muhimu mojawapo ya Broja ilikuwa filamu ya "The Pianist", yaani „Mpiga Kinanda” ya mwaka 2002, iliyoongozwa na Roman Polański na kupata tuzo tatu za Oscar na Palme d'Or kwenye Tamasha la Filamu la Cannes. Jan Krzysztof Broja pia alirekodi sauti ya kinanda kwenye sehemu ya filamu kadhaa muhimu, kama vile filamu ya "Tatarak" ya mwaka 2009, iliyoongozwa na Andrzej Wajda.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na mabalozi na wawakilishi wa biashara na mashirika ya sanaa.

Picha (9)

{"register":{"columns":[]}}