Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Tulishiriki katika Tamasha la Filamu la Ulaya nchini Tanzania

23.11.2023

Ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Filamu la Ulaya, lililoungana na Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar, tarehe 3 - 23 mwezi Novemba 2023, filamu kutoka nchi 10 za Ulaya, zikiwemo Poland na Ukraine, zilionyeshwa.

EFF_1

EFF iliandaliwa kwa mara ya tatu (ambapo kwa mara ya kwanza ilikuwa 2021) na Ujumbe wa EU na Wanachama 10 waliopo jijini Dar es Salaam: Ubelgiji, Finland, Ufaransa, Hispania, Ireland, Ujerumani, Italia, Poland, Sweden na Ukraine na kuwasilisha filamu Dar es Salaam, Morogoro na Bagamoyo.

Wawakilishi wa Ubalozi wetu walishiriki katika uzinduzi wa Tamasha hilo katika Taasisi ya Ufaransa, ambapo filamu ya Kitanzania, "Eoni", iliyoshinda Tuzo ya filamu bora ZIFF mwaka huu, ilionyeshwa.

Maonyesho ya Filamu Naszą ojczyzną jest pamięć/Memory is our homeland, yaani "Kumbukumbu ni Nchi Yetu", yalifanyika tarehe 8 Novemba katika Taasisi ya Goethe. Filamu hii ya kidokumentari ya muongozaji wa filamu kutoka Canada mwenye asili ya Kipoland, Jonathan Kołodziej Durand, inasimulia hadithi ya Wapolandi waliofukuzwa kutoka kwao kwenda Umoja wa Kisovyeti wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, kisha wakelekea Afrika kama wakimbizi mnamo mwaka 1942. Miongoni mwa Wapolandi waliopata hifadhi kutokana na ukatili wa vita alikuwa ni bibi wa muongozaji wa filamu hiyo ambae aliishi katika kambi ya wakimbizi kutoka Poland huko Tengeru, Arusha, wakati Tanganyika (Tanzania) ilikuwa chini ya Uingereza.

Sambabma na maonyesho ya filamu, tuliwasilisha maonyesho kuhusu wakimbizi kutoka Poland nchini Tanzania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Balozi Krzysztof Buzalski na wafanyikazi wa Ubalozi, pamoja na wawakilishi wa kidiplomasia na watazamaji mbalimbali.

Balozi Krzysztof Buzalski pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi pia walishiriki katika maonyesho ya filamu ya Kiukreni ya „Luxembourg Luxembourg” katika Taasisi ya Goethe.

Picha (5)

{"register":{"columns":[]}}