Tulitembelea Makaburi ya Poland huko Tengeru
06.08.2024
Naibu Konseli wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Krystyna Fatyga, alipotembelea makaburi ya wakimbizi wa Poland yaliyopo Tengeru pamoja na washiriki wa Kongamano la Dunia la Kiesperanto, lililofanyika mwaka huu jijini Arusha.
Katika ziara yake kwenye sehemu kubwa ya mazishi ya raia w Poland nchini Tanzania, iliyohifadhiwa vizuri zaidi katika bara la Afrika, lililoko mkoani Arusha, Naibu Konseli Krystyna Fatyga, anayewakilisha Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, aliwaeleza historia la eneo hilokwa wageni kutoka Poland. Makaburi hayo ni sehemu ya mapumziko ya wahamiaji 150 wa Poland waliohamishwa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ambao walifuatana na jeshi la Jenerali Anders katika safari yake ya kutoka Umoja wa Kisovieti hadi Iran na Palestina, na baadaye kusafirishwa na kuwekwa katika makoloni ya Waingereza, yakiwemo maeneo iliyokuwa Tanganyika nasasa Tanzania. Walianzisha makazi ya Wapoland, kubwa zaidi kati ya hayo yalikuwa Tengeru, yenye wakazi wapatao 5,000. Mwishoni mwa miaka ya 1940 na mwanzoni mwa miaka ya 1950, baadhi yao walihamia Uingereza, Marekani, Kanada, Australia na nchi zingine, na wengine wakibaki Tanzania.
Ubalozi unatunza sehemu sita za makaburi ambapo zamezikwa raia walioandamana na Jeshi la Anders na kufika Tanganyika mnamo mwaka 1942.