Tumesherekea miaka 233 tangu kupitishwa kwa Katiba ya Mei 3 nchini Poland na miaka 20 tangu Poland kujiunga na Umoja wa Ulaya
03.05.2024
Wakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Mei na kufafanua zaidi kuhusu historia ya Poland pamoja na mafanikio ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo baada ya kujiunga na Umoja wa Ulaya mnamo Mei 1, 2004. Pia, alisisitiza uimara wa mungano na Ukraine inayojihami dhidi ya mashambulizi ya Urusi huku ikipigania kujiunga na ulimwengu wa kidemokrasia.
Pia, hotuba ya Balozi ilizungumzia kuhusu hali nzuri ya mahusiano kati ya Poland na Tanzania, ziara ya Rais Andrzej Duda jijini Dar es Salaam mnamo Februari mwaka huu, pamoja na utekelezaji wa miradi ya pamoja, ikiwemo miradi ya maendeleo.
Hafla hiyo, ilyokuwa na chakula cha Kipolishi, iliwakusanya wageni wengi ikiwa pamoja na viongozi wa serikali ya Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, wanadiplomasia, Wapoland na wahitimu wa vyuo vikuu vya Poland nchini Tanzania. Balozi Buzalski alizungumza kwa lugha za Kipolishi, Kiingereza na Kiswahili, ambazo zilipokelewa vizuri na kuthaminiwa na wageni waliohudhuria.
Maadhimisho pia yalitoa fursa ya kutazama maonyesho ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini iliyofadhiliwa na msaada wa Polish Aid na kuwasikiliza wanamuziki kutoka Poland; Cezariusz Gadzina mwenye saksofoni na Anna Ciborowska aliyecheza kinanda; walicheza muziki ya wasanii kama Frederic Chopin na Krzysztof Komeda.