Tunaendelea kulinda mazingira na kukuza ujasiriamali katika Bonde la Kilombero na Milima ya Udzungwa
06.12.2023
Balozi Krzysztof Buzalski alitembelea maeneo ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam imekuwa ikiunga mkono shughuli za STEP, shirika lisilo la kiserikali, linaloweka jitihada ya kutengeneza mazingira ya amani baina ya watu na tembo katika Bonde la Kilombero na kuboresha ujasiriamali wa jamii za mitaa. Kipya katika mradi wa mwaka huu ni msaada wetu kwa mamlaka za Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa.
Kwa miaka kadhaa sasa, lengo la kushiriki kwa Ubalozi wa Poland katika Bonde la Kilombero limekuwa kuunga mkono shughuli za mitaa ili kukuza na kuboresha ufumbuzi la kuishi kwa amani baina ya wanyama pori na jamii, kwa kuzingatia changamoto za upanuzi wa maeneo ya makazi na kilimo zinazoingia katika maeneo wa wanyama pori, ikiwemo kando ya mipaka yaliopo chini ya hifadhi.
Mwaka huu, kwa kutumia mfuko wa fedha za Polish Aid, Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam umeshiriki katika ukarabati na upanuzi wa uzio kadhaa zinazolinda mashamba ya mazao dhidi ya uvamizi wa tembo, na umeunga mkono kuendeleza programu ya elimu juu ya kuishi kwa amani baina ya watu na tembo iliyowasilishwa kwa wanafunzi wa zaidi ya shule 20 katika kanda. Pia Ubalozi umeunga mkono kuanzishwa kwa Vyama vya Akiba na Mikopo vya Vijiji (yaani Village Savings and Loans Associsations [VSLA]). Shughuli hii ya elimu ya kifedha huleta faida kwa wakulima, kwani inawawezesha kufanya shughuli mbalimbali, kama, kupata mikopo kwa riba za chini, ambazo zinawawezesha, kwa mfano, kujizuia kuuza mazao yao hadi pale yatakapofikia thamani ya juu zaidi kwenye soko.
Pamoja na hayo, kwa mara ya kwanza mwaka huu, tumetumia mfuko wa Polish Aid kuwapatia mafunzo waongozaji wanaofanya kazi katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa na kuiunga mkono mamlaka za hifadhi katika kusafisha njia ndefu watakayotumia watalii ili konyesha kuwa mkoa ina maeneo ya kuvutia kwa watalii wa ndani na wa nje ya nchi.
Wakati wa ziara yake katika maeneo ya mradi, Balozi Krzysztof Buzalski alikutana na Mkurugenzi wa Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa Abel Mtui, timu ya walinzi wa mbuga za Tanzania, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa ni pamoja na STEP (Southern Tanzania Elephant Program), Reforest Africa, Associazzione Mazingira na ushirika wa waongozaji wa hifadhi, ambao, wamepata mafunzo ya kutoa huduma ya kwanza kwa watalii wanaokuja mbugani, kutokana na mfuko wa Polish Aid.