Tunaendelea kusaidia jamii ya albino nchini Tanzania
22.08.2024
Matatizo ya kiafya, ukosefu wa elimu stahiki na ujuzi wa kitaalamu unaowakwamisha kupata ajira, pamoja na kutengwa na jamii, bado ni changamoto kubwa zinazowakabili watu wenye ualbino nchini Tanzania. Mradi wa ‘Mustakabali bora kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania’ unaofadhiliwa na Polish Aid kimsingi unalenga kuwapa watu hao nafasi sawa za kuishi maisha bora.
Mradi wa mwaka huu wa ‘Mustakabali bora kwa watu wenye ualbino nchini Tanzania’ (yaani, Better future for people with albinism in Tanzania) ni mwendelezo wa miradi miwili ya awali iliyotekelezwa chini ya usaidizi wa maendeleo wa Poland katika miaka ya 2021-2022. Inajumuisha shughuli za kukabiliana na uhasama dhidi ya watu wenye ualbino, unyanyapaa wao na kutengwa kwa jamii. Mradi pia unalenga kuimarisha ujasiriamali na ubunifu miongoni mwa vijana wenye ualbino, ili wawe na mwanzo mzuri katika soko la kazi huko mbeleni. Aidha, mradi huo ni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa matibabu ya saratani kwa watu wenye ualbino, kwa kuzingatia kiwango kikubwa cha udzaifu ya watu hao katika kupata saratani.
Mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa Polish Aid na ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, na wadau wengine wa nchini na kutoka Poland, pamoja na Shirika la Tanga House la watoto na vijana wenye ualbino lililopo wilaya ya Bwiru jijini Mwanza kwenye mwambao wa Ziwa Victoria, ambayo inaendeshwa na Shirika la Mitume wa Afrika (Society of African Missions).
Shughuli zilizofanyika hadi mwaka 2024 ni pamoja na: semina za ualbino zilizoandaliwa Juni na Julai katika shule tatu za Mwanza (Bwiru Boys, Bwiru Girls na Shule ya Sekondari ya Montessori Maria), warsha za ujasiriamali, ubunifu, biashara na huduma za afya kwa wakazi wa Tanga, pamoja na masomo ya fidia ya Kiingereza, hisabati na sayansi ya kompyuta kwa vijana wa eneo hilo. Mnamo Juni 13 ilifanyikaSiku ya Kimataifa ya Uhamasishaji kuhusu Ualbino ambayo likuwa ni mkutano wa watoto na vijana 160 wanaoishi katika kitongoji cha Tanga House na ililenga kuwaunganisha na kuwasaidia kukabiliana na ubaguzi dhidi yaya watu wenye ualbino.
Shughuli zingine zilizopangwa kufanywa mwaka huu chini ya mradi huo ni kuandaa kozi ya ushonaji nguo kwa watu wenye ualbino ili kuwasaidia kupata ujuzi mpya muhimu itakayowasaidia katika soko la ajira.
[Picha: Tanga House SMA]