Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Tunafanya kazi kuongeza ujasiriamali wa wakazi wa Usandawe na kulinda sanaa ya miamba katika Hifadhi ya Swaga Swaga

21.01.2022

Shukrani kwa ushiriki wa mwanaakiolojia wa Poland Maciej Grzelczyk na ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa mwaka 2021 mradi uliotekelezwa kama sehemu ya misaada ya Kipolandi yenye lengo la kuamsha na kuelimisha wakazi wa eneo la Usandawe nchini Tanzania kwa ajili ya kulinda sanaa ya miamba na urithi wa kitamaduni wa jamii ya Wasandawe umekamilika.

Swaga_Swaga 2022_3

Iko katikati mwa Tanzania, eneo la Usandawe lina maeneo mengi ya sanaa ya miamba. Michoro hiyo ilitengenezwa na mababu wa wenyeji wa sasa wa mkoa huo: Wasandawe. Jumii hii kwa sasa ina idadi ya watu elfu 15-20, ambao picha za kuchora katika hali nyingi huonekana kama ishara za fumbo zinazothibitisha uwepo wa mababu zao. Umuhimu wa sanaa ya miamba katika mkoa wa Usandawe nchini Tanzania kwa ulimwengu wa kisayansi na urithi wa kitamaduni ni wa thamani sana, hata hivyo wanajamii wa Usandawe wenyewe hawana ujuzi wa kimsingi kuhusu picha za uchoraji, na bila kukusudia huchangia uharibifu wake. Mradi unaotekelezwa kama sehemu ya msaada wa Kipoland unalenga kubadilisha hali hii ya mambo. Ili kumaliza hili ni muhimu kukuza elimu ya wenyeji wa eneo hilo, kutoka kwa wadogo hadi kwa wawakilishi wa mamlaka za mitaa.

Kwa sasa, jamii ya Wasandawe wanaishi kwa kulima na kuchunga mifugo pekee. Wakati huo huo, eneo la utekelezaji wa mradi liko umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Tanzania - Dodoma, ambapo idadi ya wageni wa ndani na nje inaongezeka kila mwaka. Kwa hivyo SwagaSwaga ni hifadhi ya asili na kivutio cha watalii ambacho ni karibu zaidi na mji mkuu wa nchi. Hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa idadi ya wageni mahali hapa katika miaka ijayo.

Katika muundo wa mradi huo, madarasa ya umuhimu wa urithi wa kitamaduni wa michoro ya miamba yalifanyika kwa wanafunzi kutoka shule nane katika eneo linalozunguka Kwa Mtoro. Madarasa hayo yalikaribishwa na walimu ambao mara nyingi walionyesha shukrani zao kwa kuthamini utamaduni wa wenyeji, ambao mara nyingi huonwa kuwa wa thamani ya chini nchini Tanzania. Mafunzo kwa wafanyakazi wa hifadhi ya SwagaSwaga pia yalifanyika na yaliandaliwa maonyesho ya picha, ambayo kwa sasa yapo kwenye mamlaka ya hifadhi. Zaidi ya hayo, taarifa nyingi na vifaa vya utangazaji, ikiwa ni pamoja na mabango, vipeperushi, T-shirt na mifuko ya matangazo, vilitengenezwa na kusambazwa. Wanawake wa eneo hilo walishiriki katika utayarishaji wa baadhi ya nyenzo hizi za utangazaji. Kwa hiyo, kundi la wakazi wa eneo hilo kilipata ujuzi ambao utawawezesha kuwa na kazi za mikono (mfano; karatasi za kutengenezwa kwa mikono) na kufaidika kutokana na shughuli hizo katika siku zijazo. Kutokana na mradi huo, wakazi wa mkoa wa Usandawe watapata uwezekano mkubwa wa kupata mapato halisi kutokana na utalii.

Picha (4)

{"register":{"columns":[]}}