Tunaunga mkono maendeleo ya ujasiriamali wa wasichana na wanawake kutoka Milima ya Usambara nchini Tanzania
09.12.2023
Kama sehemu ya miradi ya maendeleo ya mwaka huu iliyofadhiliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Poland huko Dar es Salaam, kupitia mfuko wa Polish Aid, kiwanda cha kukausha matunda kinajengwa katika Milima ya Usambara. Mradi huo pia ununga mkono elimu ya ufundi kwa wanawake vijana na kusaidia kutengeneza mazingira ya kupata elimu na ujuzi, pamoja na kuchochea maendeleo ya ujasiriamali kwa kuwaongeza nafasi ya kupata ajira.
Takwimu zinaonyesha kuwa katika eneo la kijiji cha Mtae katika Milima ya Usambara nchini Tanzania, ni asilimia 14-20 tu ya watoto wanafaulu mitihani ya kumaliza elimu ya shule ya msingi. Watoto wengi (wenye umri wa miaka 13-14) hawamalizi shule na hawana taaluma yoyote ambayo ingewawezesha kujipatia kipato. Hali hii inawagusa hasa wasichana vijana, ambao hali yao ni ngumu zaidi.
Wakati katika eneo hilo ajira kama udereva wa pikipiki, uzaji wa duka na ukulima ni kazi mbazo kwa asilimia kubwa zinafanywa hasa na wanaume, ambapo mustakabali wa msichana wa kawaida unaendelea kuwa ndoa ya mapema (mara nyingi kabla ya kufika umri wa miaka 18) na uzazi - ambapo mara nyingi unahusisha ujauzito wa hatari kwa maisha na afya. Wanawake mara nyingi wanawategemea kifedha wanaume - isipokuwa mauzo madogo ya rejareja katika masoko - na hawana matarajio halisi ya kujiendeleza au kuwa huru.
Lengo kuu la warsha (kiwanda) ni kutoa aina ya ajira kwa wasichana na wanawake ambao hawajamaliza elimu ya shule ya msingi. Hivyo, warsha hiyo inakusudia kuwapatia nafasi ya kujiendeleza kibinafsi na kupata uhuru wa kifedha, lakini pia kuongeza fursa zao za kushiriki katika maendeleo ya kiuchumi la kanda. Aidha, uzalishaji na usambazaji wa mara kwa mara wa matunda unatoa pia fursa ya kipato kwa wanawake wanaouza matunda katika eneo la Mtae.
Jengo la kiwanda linapaswa kukamilika ifikapo mwisho wa mwaka huu, kwani kazi za ujenzi tayari zipo katika hatua za juu. Vifaa vinavyowezesha kuanza uzalishaji tayari vimenunuliwa, na, mipango ya kutoa mafunzo ya ujasiriamali, masoko na uhasibu kwa kikundi cha utawala yamefanywa. Mafunzo ya matumizi ya mashine ya kukausha matunda kwa washiriki wa mradi yatafuata karibuni. Uzalishaji utaanza chini ya usimamizi ya waratibu wa mradi pale ambapo matunda ya embe yatakapoonekana sokoni (mwanzoni mwa Desemba).
Eneo la mradi lilitembelewa na mwakilishi Ubalozi wa Jamhuri ya Poland, Bw. Wojciech Łysak ambaye alikutana na waratibu: Bi. Dagmara Ikiert na Bw. Abdulkadir Kaniki, pamoja na wasichana na wanawake kutoka Milima ya Usambara wanaofanya kazi kwenye mradi na wale wanaojitolea kutoka Poland. Aliwapongeza kwa kujitolea kwa kiwango kikubwa katika mradi huo.