Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Ufunguzi wa Kongamano la Kiesperanto la Dunia nchini Tanzania kwa Ushiriki wa Mwakilishi wa Ubalozi.

07.08.2024

Kongamano la Dunia la Kiesperanto lililofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 3-10 mwaka huu, limewakutanisha zaidi ya wazungumzaji mia saba sabini wa lugha ya Esperanto kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Ufunguzi wa tukio hili la kipekee, lenye lengo la kukuza uelewa wa kimataifa na kubadilishana utamaduni, pia ulihudhuriwa na mwakilishi wa ubalozi wetu - Naibu Konseli Krystyna Fatyga.

Esperanto1

Zaidi ya watu ishirini kutoka Poland walishiriki katika Kongamano hilo.. Wakati wa hafla ya ufunguzi, wazungumzaji walisisitiza jukumu ya lugha ya Eesperanto kama chombo kinachounganisha watu nje ya mipaka ya taifa, lugha na utamaduni. Pia waliangazia umuhimu wa Kongamano la Kiesperanto kama jukwaa la kukuza umoja na ushirikiano - maadili yanayopendwa na aliyebuni  lugha hiyo, Ludwik Zamenhof. Washiriki wa Kongamano, wanaowakilisha nchi mbalimbali, walihimizwa kuzingatia maadili haya, ambayo yanaunda msingi wa harakati za Esperanto. Hafla hiyo, ambayo ufunguzi wake ulihudhuriwa pia na Naibu Konseli Krystyna Fatyga kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, haikuwa tu fursa ya kujenga uhusiano wa karibu kati ya washiriki wake, lakini zaidi ya yote, jukwaa la kujadili jukumu ya lugha yaEsperanto katika kujenga uelewano na mshikamano wa kimataifa.

Picha (2)

{"register":{"columns":[]}}