Uhalalishaji
Uhalalishaji ni uthibitisho kwamba hati imetolewa na ofisi sahihi. Kwa njia ya uhalalishaji ofisa wa konsula anathibitisha ukweli wa saini na mhuri wa ofisa wa kigeni. Hii inakuruhusu kutumia hati za kiofisi za kigeni Poland.
Uhalalishaji unafanyika kwenye nchi zisizo-wanachama wa The Hague Convention Abolishing the Requirement of Legalisation for Foreign Public Documents ya Oktoba 5, 1961 (Journal of Lawskwenye jarada la sheria ya 2005, namb. 112, kipengere cha 938).
Konsula ya Poland Tanzania inahalalisha hati zinazotolewa Tanzania, Rwanda na Comoros
Tafadhali kumbuka! Konsula inaweza kuhalalisha hati ambazo ni orijino kopi za kiofisi. Photokopi na hati zilizotolewa kopi haziwezi kuhalalishwa. Ni lazima hati zithibitishwe na mamlaka ya ngazi za chini (serikali za mtaa) kabla hujaziwasilisha kwa konsula. Katika nchi nyingi uthibitishwaji unafanywa na Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya haki au mamlaka nyingine ya serikali kuu ya hati orijino ya nchi
Konsula itakataa kuhalalisha hati isiyo na utangulizi wa uhalalishwaji.
Weka miadi kwenye ubalozi, chagua miadi ya masuala ya kisheria kwenye tovuti ya e-Konsulat, piga simu au tuma barua pepe kwenye ofisi ya konsula husika.
Ada ya uhalalishaji ni USD 32.
Kama mamlaka ya nje inahitaji uhalalishaji wa hati Poland, tafadhali soma taarifa kwenye Polish MFA website.