Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Wawakilishi wa Ubalozi walitembelea makaburi ya Kipoland nchini Tanzania kwenye hafla ya Siku ya Watakatifu Wote

01.11.2022

Katika maadhimisha ya siku ya Watakatifu Wote, Balozi Krzysztof Buzalski na wawakilishi wa Ubalozi huo waliweka maua kwenye makaburi ya wananchi wenzao kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati Balozi msaidizi Piotr Kruze alitembelea Necropolis kubwa zaidi katika Afrika ya iliyopo Tengeru na makaburi ya Kondoa na Ifunda

Tengeru 2022_1

Ubalozi unatunza maeneo 6 ya makaburi nchini Tanzania yenye makaburi ya Wapoland waliokuwa uhamishoni. Mnamo mwaka 2018-2021 Ubalozi ulifanya matengenezo au ukarabati wa mawe mengi ya makaburi ya Poland katika makaburi matano, mipango ni kukarabati makaburi ya sita (ya mwisho).

Makaburi makubwa zaidi ya Wapolandi nchini Tanzania na wakati huohuo barani Afrika ni makaburi ya Tengeru, ambapo zaidi ya watu 150 waliohamishwa kutoka Poland kutoka Vita vya Pili vya Dunia wamezikwa. Walikuwa ni raia waliofuatana na jeshi la Jenerali Anders wakati wa safari yake kutoka Umoja wa Kisovieti hadi Iran na Palestina, kisha wakasafirishwa na kuwekwa katika makoloni na maeneo ya Waingereza, likiwemo eneo la iliyokuwa Tanganyika kwa wakati huo. Walianzisha makazi ya Wapolandi hapa, Makazi makubwa zaidi ambayo yalikuwa Tengeru (takriban makazi 5,000). Mwanzoni mwa miaka ya 1940 na 1950, baadhi yao walihamia Uingereza, Marekani, Kanada, Australia na nchi nyingine, lakini wengine walibaki Tanzania.

Picha (8)

{"register":{"columns":[]}}