Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Jakub Wiśniewski nchini Tanzania
13.12.2024
Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland Jakub Wiśniewski nchini Tanzania tarehe 11-12 Desemba 2024, iliruhusu kubadilishana mawazo na wawakilishi wa mamlaka za Tanzania kuhusu uwezekano wa ushirikiano wa maendeleo, uwekezaji na biashara kati ya Poland na Tanzania. Pia ilikuwa ni fursa ya kukutana na wanufaika wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa jijini Dar es Salaam kwa mfuko ya Polish Aid.
Katika ziara yake jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland Jakub Wiśniewski amekutana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji wa Tanzania Stanslaus Nyongo, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri, Balozi John Ulanga - Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, na balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, aliyeidhinishwa pia na Poland - Hassan I. Mwamweta. Mwakilishi wa serikali ya Poland alisisitiza kuwa Tanzania ni kati ya washirika anaopewa kipaumbele na Poland chini ya mpango wa Polish Aid. Tunafanya kazi kwa karibu na Tanzania katika sekta za afya, bayoanuai, mabadiliko ya hali ya hewa, elimu na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na sekta ya ujasiriamali, tukilenga zaidi kuwapatia vijana ujuzi unaohitajika katika soko la ajira la Tanzania. Kwa upande wa Tanzania, mkutano huo ulikuwa ni fursa kuwasilisha kwa wajumbe wa Polandi vipaumbele vya Serikali ya Tanzania kwa miaka ijayo, vikiwemo maendeleo katika sekta ya kilimo, afya, usimamizi wa maliasili, ujasiriamali na ulinzi wa bayoanuai.
Katika ziara hiyo nchini Tanzania, Naibu Waziri Jakub Wiśniewski pia alifanya kikao na Mkuu wa Umoja wa Ulaya jijini Dar es Salaam, Balozi Christine Grau, kuhusiana na uwezekano wa Poland kushiriki zaidi katika shughuli za Timu ya Ulaya katika nyanja ya kimaendeleo na Tanzania. Suala la uwezo mkubwa wa Tanzania kushirikiana na wawekezaji wa nje pia lilijadiliwa.
Aidha, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Polandi, Jakub Wiśniewski alitembelea shule ya chekechea ya "St. Angels Day Care Center" inayoendeshwa na Usharika wa Masista wa Mary Immaculate (pamoja na masista wa Poland) iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, ambayo mwaka 2021 ilinufaika na ruzuku ndogo kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ununuzi wa chombo cha usafiri ili kuboresha usalama wa wanafunzi wake, pamoja na Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe kilichopo Segerea kinachoendeshwa na mapadre wa Kipolish Wafransisko. Kitu hicho kinhudumia zaidi ya watoto na vijana 1,800 katika hatua mbalimbali za elimu ya shule - kutoka chekechea hadi shule za sekondari na ufundi - na imejikuta miongoni mwa wanufaika wa misaada ya maendeleo ya Poland mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni, ikipokea fedha kwa ajili ya ujenzi na vifaa vya chekechea na shule ya ufundi, na pia ya ununuzi wa kompyuta ya maabara ya IT.
Naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Poland pia alitembelea enel la mradi uliofadhiliwa na Msaada wa Poland na unaoitwa Climate Action for Food and Education Project for People with Albinism, yaani Hatua ya Hali ya Hewa kwa Chakula na Elimu Mradi kwa Watu wenye Albino, ambao umekuwa ukifanywa na ADRA Poland kwa kushirikiana na ADRA Tanzania. Lengo la mradi ni kuboresha maisha ya wanawake kutoka jamii ya albino nchini Tanzania kwa kuwasaidia kupata na kukuza ujuzi ambao unawaruhusu kupata ajira au kuanzisha biashara zao katika sekta wa kilimo, hasa kilimo na uuzaji wa mboga na matunda. Naibu Waziri Jakub Wiśniewski alipata fursa ya kuzungumza na wawakilishi wa ADRA na wawakilishi wa Jumuiya ya Albino Tanzania, pamoja na kundi la wanufaika wa mradi.
Kutembelea kwa Warizi nchini Tanzania pia ilikuwa fursa ya kuona Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ambayo imekuwa ikinufaika na vifaa na mafunzo kwa watumishi katika fani ya huduma za dharura za matibabu ikiwa ni sehemu ya mradi wa miaka mitatu unaoitwa “Support for the Emergency Medicine Sector in the Dar es Salaam Region”- Msaada kwa sekta ya dawa za dharura katika mkoa wa Dar es Salaam” unaotekelezwa na Taasisi ya Polish Centre for International Aid (PCPM) kwa ushirikiano na Aga Khan Health Service Tanzania (AKHST) na serikali ya Tanzania, inayofadhiliwa na Polish Aid, pamoja na Kituo cha Mafunzo ya Dharura cha Tanzania-Poland, ambacho kiliundwa kutokana na ufadhili wa mradi uliotajwa hapo juu. Kituo cha Mafunzo ya Dharura cha Tanzania na Poland ni kituo tangulizi nchini Tanzania ambacho kinatofautiana na vituo vingine vya aina yake kutokana na vifaa vyake vya kisasa vya kufundishia, mbinu bunifu za kufundishaji, na ulinganishaji wa kimkakati na vipaumbele vya afya vya kitaifa na kimataifa. Inafaa kuongeza kuwa huduma za matibabu ya dharura nchini Tanzania ni taaluma mpya, ambayo mfumo wake bado unaundwa, na mfumo mzima wa matibabu ya dharura katika nchi hii bado unaundwa.
Kukaa nchini Tanzania pia ilikuwa fursa ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ambayo imekuwa ikinufaika na vifaa na mafunzo kwa watumishi katika fani ya huduma za dharura za matibabu ikiwa ni sehemu ya mradi wa miaka mitatu unaoitwa “Support for the emergency medicine sector in the Dar es Salaam region “- Msaada kwa sekta ya dawa za dharura katika mkoa wa Dar es Salaam” unaotekelezwa na Taasisi ya Polish Centre for International Aid (PCPM) kwa ushirikiano na Aga Khan Health Service Tanzania (AKHST) na serikali ya Tanzania, inayofadhiliwa na Polish Aid, pamoja na Kituo cha Mafunzo ya Dharura cha Tanzania-Poland, ambacho kiliundwa kutokana na ufadhili wa mradi uliotajwa hapo juu pia. Kituo cha Mafunzo ya Dharura cha Tanzania na Poland ni kituo tangulizi nchini Tanzania ambacho kinatofautiana na vituo vingine vya aina yake kutokana na vifaa vyake vya kisasa vya kufundishia, mbinu bunifu za kufundishia, na iliyo na mikakati inayofuata vipaumbele vya afya vya kitaifa na kimataifa. Inafaa kuongeza kuwa huduma za matibabu ya dharura nchini Tanzania ni taaluma mpya, ambayo mfumo wake bado unaundwa, na mfumo mzima wa matibabu ya dharura nchini bado unaundwa.