Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.
Kwenda Nyuma

Ziara ya Utafiti ya Mwandishi wa Habari wa Tanzania, Bwana Charles Makakala nchini Poland

30.06.2023

Kuanzia tarehe 19 hadi 24 Juni 2023, mwandishi wa habari mashuhuri Tanzania, Bw. Charles Makakala, alitembelea Warsaw, Lublin na Gdansk kama sehemu ya ziara ya utafiti iliyoandaliwa na ubalozi wa Poland nchini Tanzania. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kushuhudia mafanikio na maendeleo nchini Poland, misaada inayotolewa na Poland na Wapoland kwenda nchini Ukraine inayopigana vita dhidi ya Urusi, na kumwonyesha mbinu za taarifa potofu za Urusi. Pamoja na hayo, Bw. Charles Makakala aliona shughuli za makampuni ya Kipoland kutoka sekta ya teknolojia ya kisasa zinazovutiwa kushirikiana na Tanzania.

Wizyta_w_PL_dzienikarza_TZ 2023_0

Mjini Warsaw, Bw. Charles Makakala alianza ziara kwa kutembelea Makumbusho ya Uasi wa Warsaw, baadae akakutana na wawakilishi wa kampuni ya LUG, ambayo inashughulika na mifumo ya kisasa ya taa za mijini. Katika siku zilizofuata, alikutana na wawakilishi wa timu ya mawasiliano ya kimkakati katika Ofisi ya Msemaji wa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Kituo cha Elimu cha Msaada wa Kimataifa Poland. Pia alitembelea makao makuu ya Caritas Poland na Wizara ya Maendeleo na Teknolojia na Chama cha Biashara cha Taifa. Aliweza pia kutana na Asseco Poland, Shirika la Taifa la Kubadilishana Wasomi, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Warsaw, na Shule Kuu ya Biashara. Mwandishi wa habari huyo, pia, alipata nafasi ya kutembelea Makumbusho ya Taifa, Ngome ya Kifalme na sehemu ya mji wa zamani (yaani Old Town).

Mjini Lublin, mwandishi wa habari alipata nafasi kukutana na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Marie Curie-Skłodowska na Programu ya Study in Lublin, baadae akatembelea Makumbusho ya Majdanek, Ngome ya Lublin na sehemu ya mji wa zamani.

Mjini Gdansk, Bw. Charles Makakala alitembelea, pamoja na Balozi Krzysztof Buzalski, Kituo cha Mshikamano cha Ulaya, Nyumba ya Zamani ya Mikutano ya Artus, Kanisa la Mariacki na sehemu ya mji wa zamani wa Gdansk.

Bw. Charles Makakala aliandika nakala nzuri sana juu ya ziara yake nchini Poland kwenye gazeti la The Citizen na kwenye akaunti yake ya Twitter @makakalajr .

Picha (11)

{"register":{"columns":[]}}