Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.

C-Type Viza ya Schengen

Ni wapi kwa kutuma maombi?

Unaweza kutuma kwenye ofisi ya Konsula - 15 Mtwara Road, Oysterbay, Msasani.

Je natakiwa kupeleka maombi kwa mikono?

Fomu ya maombi ya Viza lazima iwasilishwe kwa mikono. Misheni ya Diplomasia haipokei maombi yatumwayo kwa njia ya fax, barua za kawaida au barua pepe.

Namna gani ya kuomba miadi?

Unaweza kuomba miadi ya kutuma maombi ya viza kwenye mfumo wa e-konsulat, tarehe zipo katika utaratibu wa kawaida.

Ni taarifa gani ninazozihitaji ili kuwasilisha?
  1. Fomu ya maombi ya viza iliyojazwa kupitia mfumo wa e-konsulat, iliyochapishwa na kusainiwa.
  2. Picha ya rangi yenye ukubwa wa cm 3.5x4.5. Picha lazima iwe:
  • Kali, yenye kitambaa cheupe kwa nyuma (back ground) na iliyochapishwa kwenye karatasi lenye ubora,
  • Mpya isiyozidi miezi 6 iliyopita,
  • Iliyochukuliwa usoni ikionyesha macho vizuri na uso kutoka pande zote mbili kutokea juu kwenda mpaka kwenye mabega, na uso ukiwa unaonekana kwa asilimia 70-80% ya picha yote. Picha inatakiwa ipigwe bila kuvaa kitu chochote kichwani.
  1. Pasipoti iliyotolewa ndani ya miaka, iwe halali mpaka angalau miezi mitatu kabla ya tarehe ya mategemeo ya kurudi na ikiwa na angalau na nafasi za kurasa mbili kwa ajili ya viza. Ikiwa una pasipoti nyingine ambayo ni halali, unapaswa uiambatanishe kwenye fomu ya maombi ya viza.
  2. Nakala ya ukurasa wa pasipoti wenye taarifa binafsi na picha.
  3. Bima ya afya iliyohalali kutumika katika nchi zote za eneo la Schengen kwa kiwango kisichopungua EUR 30,000. Kama ukituma maombi ya viza ya multiple-entry inatakiwa ijumuishe tarehe ya kuingia kwa mara ya kwanza.
  4. Nakala ya hati ya kitambulisho kuthibitisha makazi yako ndani ya wilaya ya konsula uliyotumia maombi yako.
  5. Uthibitisho kwamba una namna ya kutosha ya kujikimu fomu iliyotolewa maamuzi na misheni:
  • Maelezo ya bank yaliyotolewa na benki yako
  • Cheti cha mapato yako kutoka kwa mwajiri wako kwa miezi mitatu iliyopita
  1. Uthibitisho wa makazi (kwa mfano mwaliko rasmi au booking ya hotel au nafasi).
  2. Taarifa ya uthibitisho wa lengo na hali ya mpango wa ukaaji wako Poland.

Nyongeza, wakati unatuma maombi ya viza kwa wadogo unatakiwa:

  • Kibali cha maandishi cha mzazi/wazazi wa mtoto kuomba viza kikiwa kimethibitishwa na mthibitishaji. Kama kuna mlezi mmoja, inatakiwa ithibitishwe na cheti cha kuzaliwa, maamuzi ya mahakama kama ulinzi wa wazazi haupo au cheti kifo cha mzazi mwingine.
  • Pasipoti orijino za wazazi na nakala (kopi)
  • Cheti cha kuzaliwa orijino na nakala (kopi)

Kama mtoto ameingizwa kwa wazazi au kwenye pasipoti ya mlezi wa kisheria, tafadhali wasilisha maombi tofauti ya viza. Viza itaingizwa kwenye pasipoti ya mzazi au mlezi wa kisheria.

Tafadhali kumbuka:

  • Lazima utume maombi yako ya viza kwenye ofisi ya konsula au konsula ya ubalozi.
  • Kwa kawaida taarifa za hapo juu zinatosha kwa mtu kupata viza, ingawa ofisa wa konsula anaweza kutaka taarifa Zaidi.
  • Tuma maombi ya viza sio mapema zaidi ya miezi mitatu kabla ya safari yako iliyopangwa.
  • Ofisa wa konsula anaweza, lakini haipaswi kuwa hivi, kumwalika mwombaji kwa mahojiano.
  • Unaweza kuzuiliwa usiingie tena kwenye nchi za Schengen kama utatuma taarifa za uongo au hati feki.
  • Kupata viza hakukupi uthibitisho wa uhakika wa kuingia nchi za eneo la Schengen-maamuzi ya mwisho huwa yanatolewa na mamlaka ya nchi unayokusudia kuvuka kwenye mpaka wa eneo la Schengen.
Inagharimu kiasi gani?

Ada ya maombi ya viza dola (USD) 86 keshi na huwa hairudishwa bila kujali maamuzi ya ofisa wa konsula.

Kuna muda gani wa kusubiri?

Ofisa wa konsula atafanya maamuzi kuhusiana na viza ndani ya siku 15 za kalenda za siku. Kwa nadra isivyo kawaida, muda wa maamuzi unaweza kuvutwa mpaka siku 30 au 60 

Namna gani ya kupata taarifa?

Baada kuwasiliana na ofisi, taarifa zinaweza kupatikana wakati wa masaa ya konsula.

Namna gani ya kukata rufaa?

Baada ya kuwasiliana na mamlaka husika, maombi ya kuomba kurudiwa yanaweza kupelekwa wakati wa masaa ya konsula.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, raia wa nchi nyingine anaweza kutuma maombi ya viza kwenye ubalozi?

Ubaolzi unaweza kupokea maombi ya viza kwa raia na wakazi wa nchi zinazotumia ubalozi huu tu. Uthibisho wa makazi unaohitajika.

Unaweza kutuma maombi ya viza kwa barua ama barua pepe?

Hapana, maombi ya viza lazima yapelekwe na mtu baada ya kuomba miadi kwenye mfumo wa e-konsulat katika mtandao (www.e-konsulat.gov.pl).

Je, ninaweza kulipa kwa njia ya benki?

Hapana, ada ya konsula inaweza kulipwa kwa pesa taslimu tu. Tafadhali uje na kiasi kilichotimia katika dola (USD) tu.

Je bima ya afya ya Poland inatosha?

Hapana, unahitajika uthibitisho wa bima ya afya kwa nchi zote za Schengen wenye kiwango cha chini EUR 30,000 na ambao unatosheleza safari yako nzima.

Je, ninahitaji kutoa uthibitisho wa tiketi ya ndege?

Hapana, booking ya ndege ya kurudi inatakiwa na maombi ya viza. Viza itatolewa kwa kipindi chote ikiwa ni pamoja na tarehe ya kufanya booking. Ununuzi wa tiketi ya ndege unaweza kufanywa baada ya viza kutolewa.

{"register":{"columns":[]}}