Viza – Taarifa za ujumla
Aina za viza
Kabla ya kutuma maombi, ni lazima uamue ni aina gani ya viza unahitaji:
Viza ya Airport transit Schengen
Chagua viza hii kama unapanga kupitia eneo la usafiri wa kimataifa wa uwanja wa ndege wa Schengen na pasipoti ya moja ya nchi hizi: Afghanistan, Bangladesh, Democratic Republic of Congo, Eritrea, Ethiopia, Ghana, Iran, Iraq, Nigeria, Pakistan, Somalia, Sri Lanka.
Viza ya Schengen (C-Type)
Chagua viza hii kama unapanga kukaa Poland au nchi nyingine ya Schengen kwa siku zisizozidi 90 kwa kila kipindi cha muda wa siku 180. Hii ina maana kwamba unaruhusiwa kisheria kukaa kwenye zone ya Schengen, kama tu ukaaji wako haujazidi siku 90 kwa siku 180 zilizopita. Kifaa maalumu cha mahesabu (Kikokotozi) kwenye tovuti ya Tume ya Ulaya na stronie Komisji Europejskiej itakusaidia kuhesabu kwamba ni kwa muda gani unaweza kukaa kwenye nchi za Schengen.
Unaweza kutuma maombi ya Viza ya Schengen kwenye misheni ya kidiplomasia ya Poland kama:
- Poland ndio nchi pekee ya safari yako katika kutembelea nchi za zone ya Schengen;
- Kama unatembelea nchi za Schengen zaidi ya moja, lakini Poland ndio sehemu yako kuu;
- Kama hujui ni nchi gani ya Schengen itakuwa nchi yako kuu ya kufikia, lakini utapitia kwenye mpaka wa Schengen kwa mara ya kwanza Poland.
Kwa kesi maalum inawezekana kutoa viza ya Schengen LTV ambayo inakubalika kwenye nchi zilizochaguliwa za Schengen.
Viza ya Taifa (National visa (D-Type)
Chagua viza hii kama unataka kukaa Poland kwa zaidi ya siku 90, utambulikanaji wa viza ya taifa hauwezi kuzidi zaidi ya mwaka mmoja. Pia unaweza kuomba viza ya taifa kama unatafuta hifadhi, kurudishwa au kama utatumia kadi ya upendeleo ya Poland (Polish Card privileges)
Utaratibu wa viza uliorahisishwa kwa ajili ya familia za wanachama wa raia wa EU
Nani anastaili?
TAARIFA MUHIMU: utaratibu huu unatumika kwa familia za mataifa wanachama wa EU ambao hawana uraia wa Poland au hawana kibali cha makazi ya kudumu Poland.
Mataifa ya EU yanajumuisha:
- Mataifa ya nchi wanachama wa EU
- Mataifa ya Iceland, Liechtenstein, Norway and Switzerland.
Mwanafamilia wa taifa mwanachama wa EU ni:
- Mwenzi
- Mwenzi ambaye taifa la EU liliuunganisha uhusiano huo chini ya sheria ya nchi hiyo, kwa kujalisha kwamba sheria ya nchi hii inautambua mfumo huo kuwa sawa na ndoa.
- Mtoto chini ya miaka 21 ambaye ni temegemezi kwenye mataifa ya EU na mwenzi wake.
Kwa utaratibu huu unastaili kuwasilisha maombi yako ya viza:
- Bila gharama yoyote
- Bila maombi ya kuomba miadi
Vitu vinavyohitajika:
- Maombi ya viza yaliyochapishwa na kusainiwa (yajazwe kwenye mtandao ( online))
- Picha ya rangi ya hivi karibuni ukubwa wa mm 35x45.
- Pasipoti halali
- Cheti cha uthibitisho wa ndoa au mahusiano cha taifa la EU,
- Cheti cha uthibitisho unamsindikiza katika taifa la EU katika safari yake au kuungana naye katika sehemu yake ya makazi.
Kukataliwa kwa Viza:
Maombi yako ya Viza yanaweza kukataliwa tu kama:
- Data zako ziko kwenye usajiri wa wageni ambao wanakaa katika nchi ya Poland hazikubaliki,
- Mamlaka ya Viza imezingatia taarifa kwamba ukaaji wako unaweza kuwa tishio kwa ulinzi wa nchi au usalama wa taifa au ulinzi wa usalama wa uma, amri na afya.
Ofisa wa konsula anakataa viza kwa njia ya maamuzi. Unaweza kukata rufaa dhidi ya kukataliwa kwa viza kwenye Wizara ya Mambo ya Nje.
Taarifa za biometriska (biometric)
Unapotuma maombi ya viza, unatakiwa kutoa taarifa zako za biometriska: picha katika viza ya taifa (national visa) na picha na alama za vidole kwenye viza ya Schengen.
Ikiwa umeshatuma maombi tuma maombi kwenye viza ya Schengen hivi karibuni ndani ya miezi 59, na kama umeshatoa alama zako za vidole, hutakiwi kuvitoa tena – mfumo utatuma taarifa zako moja kwa moja.
Waombaji wafuatao hawatakiwi kutoa alama zao za vidole:
- Watoto chini ya miaka 12
- Watu ambao kimwili hawawezi kutoa alama zao za vidole (kwa sababu hawana vidole au wanaumwa magonjwa ya vidole yasiyo ya kudumu kama kutetemeka kwa vidole)
- Kiongozi wa nchi au serikali, mwanachama wa serikali ya taifa na wenza wao na wajumbe maalumu wa kiserikali kama wamealikwa kwa malengo ya kiofisi.
- Wafalme na viongozi wa ngazi za juu wa familia za kifalme, kama wamealikwa kwa shughuli za kiofisi.
Taarifa binafsi
Mamlaka husika ya mchakato wa taarifa binafsi ambayo iko kwenye mfumo wa taarifa za Viza (VIS) ni Mamlaka kuu ya kiufundi ya Mfumo wa taarifa wa Taifa katika makao makuu ya Polisi ya Taifa, Anuani: ul. Puławska 148/150, 02-624 Warszawa.
Msingi wa Kisheria
Ustawa z dnia 14 lipca 2006 r. o wjeździe na terytorium Rzeczypospolitej Polskiej, pobycie oraz wyjeździe z tego terytorium obywateli państw członkowskich Unii Europejskiej i członków ich rodzin (Dz. U. z dnia 11 sierpnia 2006 r. poz. 1525)
Ustawa z dnia 12 grudnia 2013 r. o cudzoziemcach (Dz. U. z dnia 30 grudnia 2013 r. poz. 1650 z późn. zm.)
Ustawa z dnia 25 czerwca 2015 r. Prawo konsularne (Dz. U. z dnia 31 sierpnia 2015 r. poz. 1274)