Ili kuhakikisha huduma bora zaidi, tunatumia faili ndogo zinazoitwa kuki. Wakati wa kutumia wavuti yetu, faili za kuki zinapakuliwa kwenye kifaa chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Kwa kuongezea, utumiaji wako wa wavuti yetu ni sawa na idhini yako kwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi inayotolewa na njia za elektroniki.

Kufanya tafsiri

Wapi kwa kutuma maombi?

Unaweza kutuma maombi yako kwenye ofisi ya kunsula iliyochaguliwa inayotoa tafsiri kutoka kwenye lugha ya hati.

Je, ninatakiwa kupeleka maombi mikono?

Unaweza kuwasilisha maombi kwa mikono au kuyatuma kwa njia ya posta.

Namna gani ya kuweka miadi?

Unaweza kuweka miadi yako kupitia mfumo wa  e-konsulat /kwa simu (+255) 22 222 1050.

Ni taarifa gani ninazihitaji ili kutuma maombi?

Dokomenti ambazo unataka ofisa wa konsula kutafsiri.

Ofisa wa konsula anatafsiri dokomenti kutoka kwenye Kipoland kwenda Kiingereza na kutoka Kiingereza kwenda Kipoland.

Je, inagharimu kiasi gani?

Ada ya kutafsiri na kuthibitisha dokomenti kwa ukurasa mmoja ni USD 96 na kutafsiri na kuthibitisha dokomenti ya hali ya uraia ni USD 54.

Je, ni muda gani wa kusubiri?

Ofisa wa konsula anatafsri document bila kuchelewa vibaya, lakini sio Zaidi ya siku 30 tangu tarehe ya kujazwa.

Jinsi gani ya kupata docomenti?

Unaweza kwenda kuchukua moja kwa moja. Pia unaweza kuomba wakutumie kwa njia ya posta kama ukilipia gharama za utumaji.

Namna gani ya kukata rufaa?

Ikiwa kazi ya kutafsiri itakataliwa, ofisa wa konsula atatoa maamuzi. Unaweza kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya siku 7. Unaweza kutuma rufaa yako kwa kutumia ofisa wa konsula ambaye alitoa maamuzi.

{"register":{"columns":[]}}