Habari
-
18.12.2023Tamasha la wasanii kutoka Poland, Tanzania na Malawi katika toleo la III la Tamasha la Pamoja ZanzibarToleo la III la Tamasha la Pamoja Zanzibar lilifanyika Desemba 8-10, 2023, ambapo tamasha za muziki tatu ziliandaliwa na Radek Bond Bednarz. Mwaka huu walishiriki familia maarufu ya muziki ya Tanzania Zawose na msanii kutoka Malawi NyaGo, kwa msaada wa Ubalozi.
-
10.12.2023Kompyuta Mpya kutolewa kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea, TanzaniaWanafunzi wa shule za sekondari, ufundi, pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Elimu cha Mtakatifu Maximilian Kolbe huko Segerea, tayari wanatumia kompyuta zilizonunuliwa mwaka huu kupitia mradi uliotekelezwa kwa pamoja na kituo hicho na Ubalozi wa Poland jijini Dar es Salaam, ukiwa umefadhiliwa na msaada wa Polish Aid.
-
09.12.2023Tunaunga mkono maendeleo ya ujasiriamali wa wasichana na wanawake kutoka Milima ya Usambara nchini TanzaniaKama sehemu ya miradi ya maendeleo ya mwaka huu iliyofadhiliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Poland huko Dar es Salaam, kupitia mfuko wa Polish Aid, kiwanda cha kukausha matunda kinajengwa katika Milima ya Usambara. Mradi huo pia ununga mkono elimu ya ufundi kwa wanawake vijana na kusaidia kutengeneza mazingira ya kupata elimu na ujuzi, pamoja na kuchochea maendeleo ya ujasiriamali kwa kuwaongeza nafasi ya kupata ajira.
-
06.12.2023Tunaendelea kulinda mazingira na kukuza ujasiriamali katika Bonde la Kilombero na Milima ya UdzungwaBalozi Krzysztof Buzalski alitembelea maeneo ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam imekuwa ikiunga mkono shughuli za STEP, shirika lisilo la kiserikali, linaloweka jitihada ya kutengeneza mazingira ya amani baina ya watu na tembo katika Bonde la Kilombero na kuboresha ujasiriamali wa jamii za mitaa. Kipya katika mradi wa mwaka huu ni msaada wetu kwa mamlaka za Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa.
-
23.11.2023Tulishiriki katika Tamasha la Filamu la Ulaya nchini TanzaniaIkiwa ni sehemu ya Tamasha la Filamu la Ulaya, lililoungana na Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar, tarehe 3 - 23 mwezi Novemba 2023, filamu kutoka nchi 10 za Ulaya, zikiwemo Poland na Ukraine, zilionyeshwa.
-
11.11.2023Tuliadhimisha Sikukuu ya Uhuru nchini TanzaniaKatika tafrija ya kuadhimisha miaka 105 tangu Poland kupata uhuru, ilioandaliwa katika bustani za Ubalozi wa Poland mjini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski aliwasilisha maonyesho ya "Wanawake wa Uhuru", wakati bendi ya wamisionari wa kimataifa iliimba nyimbo za Kipolandi. Pia havikukosekana vyakula vya Kipoland vilivyoandaliwa na Ubalozi.
-
01.11.2023Ziara katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wakati wa Siku ya Watakatifu WoteSiku ya November 1, 2023, Balozi Krzystof Buzalski pamoja na wasaidizi wake walitembelea na kuweka maua katika makaburi ya Wapoland zilizopo eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ubalozi unatunza makaburi kwenye maeneo 6 nchini, yenye raia waliofuatana na jeshi la Jenerali Anders aliyewalisi Tanganyika mwaka 1942.
-
30.06.2023Ziara ya Utafiti ya Mwandishi wa Habari wa Tanzania, Bwana Charles Makakala nchini PolandKuanzia tarehe 19 hadi 24 Juni 2023, mwandishi wa habari mashuhuri Tanzania, Bw. Charles Makakala, alitembelea Warsaw, Lublin na Gdansk kama sehemu ya ziara ya utafiti iliyoandaliwa na ubalozi wa Poland nchini Tanzania. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kushuhudia mafanikio na maendeleo nchini Poland, misaada inayotolewa na Poland na Wapoland kwenda nchini Ukraine inayopigana vita dhidi ya Urusi, na kumwonyesha mbinu za taarifa potofu za Urusi. Pamoja na hayo, Bw. Charles Makakala aliona shughuli za makampuni ya Kipoland kutoka sekta ya teknolojia ya kisasa zinazovutiwa kushirikiana na Tanzania.
-
05.05.2023Maadhimisho ya miaka 232 tangu kupitishwa kwa Katiba ya Tarehe 3 Mei nchini TanzaniaWakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Mei na kufafanua zaidi kuhusu historia ya Poland na mafanikio ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.
-
26.04.2023Ubalozi utafungwa tarehe 1 na 3 Mi 2023. Upande wa viza pia utafungwa tarehe 5 MeiTunawataarifu waombaji wa visa kuwa tarehe 1 Mei ( siku ya wafanyakazi) na tarehe 3 Mei ( siku ya katiba) Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam utafungwa. Aidha, upande wa viza wa ubalozi utafungwa tarehe 5 Mei.