Habari
-
31.10.2022Masada wa Kipolishi waongeza ujasiriamali wa wanawake nchini TanzaniaWasichana kadhaa kutoka kijiji cha Mtae nchini Tanzania walishiriki katika mradi wa "Warsha ya Masista" mwaka huu, wakipata ujuzi wa kitaalamu katika fani ya ushonaji nguo. Utekelezaji wake uliwezekana kutokana na fedha za msaada wa Kipoland kama sehemu ya ruzuku ndogo iliyotolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam kwa mshirika wa ndani - A.D. View Management Ltd.
-
21.10.2022Balozi Buzalski alishiriki katika ziara ya Waziri Tax nchini PolandMnamo Oktoba 17-19, 2022, Balozi Krzysztof Buzalski alishiriki katika mikutano ya Waziri wa Mambo ya Nje Zbigniew Rau na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Stergomena Tax na katika mikutano ya SGGW na PAIH na kampuni za Poland zinazopenda kushirikiana na Tanzania.
-
19.09.2022Uzinduzi wa maonyesho ya Kipoland-Kiukreni "Mama, sitaki vita!"Mnamo Septemba 14, 2022, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam ulizindua katika Alliance Françaisean maonyesho yenye kichwa “Mama, sitaki vita! 1939-45 Poland/2022 Ukraine ”, iliyohudhuriwa na wawakilishi wa Ubalozi wa Ukraine na wageni wengi.
-
17.09.2022Tunaungana na siku ya usafishaji Duniani nchini TanzaniaJumamosi, Septemba 17, 2022, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam kwa mara nyingine tena uliungana na siku ya usafishaji Duniani nchini Tanzania.
-
21.06.2022Hotuba na maonyesho juu ya Wapoland wa uhamishoni waliokuwa Tanganyika katika Chuo Kikuu cha Jordan, MorogoroBalozi msaidizi wa Jamhuri ya Poland Piotr Kruze alishiriki katika mdahalo kuhusu historia ya Vita vya Pili vya Dunia katika Chuo Kikuu cha Jordan kilichopo Morogoro na kuwasilisha maonyesho ya Wapoland wa uhamishoni waliokuwa Tanganyika.
-
17.05.2022Maonesho ya Elimu ya Umoja wa Ulaya jijini Dar es SalaamUbalozi wa Poland ulishiriki kikamilifu katika Maonesho ya Elimu ya Umoja wa Ulaya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ulaya nchini Tanzania yaliyoandaliwa na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya.
-
15.05.2022Maadhimisho ya Siku ya Ulaya nchini TanzaniaMnano tarehe 9 Mei, 2022, tuliadhimisha Siku ya Ulaya jijini Dar es Salaam. Katika tafrija hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje, LiberataMulamula, Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na wageni mbalimbali, maonesho ya picha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini Tanzania na Nchi Wanachama yaliwasilishwa.
-
07.05.2022Maadhimisho ya miaka 231 tangu kupitishwa kwa Katiba ya Tarehe 3 Mei na siku ya Wapoland waishio nchini TanzaniaWakati wa tafrija iliyoandaliwa katika bustani za Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alirejelea historia ya kupitishwa kwa Katiba ya tarehe 3 Me na kusoma barua kutoka kwa Waziri SzynkowskivelSęk yenye pia ujumbe wa kuwatakia kila la kheri wakazi wote wenye asili ya Kipoland waishio nchini.
-
06.04.2022Msaada wa Kipoland unasaidia kuboresha elimu, usafi na mazingira ya usafi wa jamii katika eneo la KiabakariUpande wa Kaskazini – Magharibi mwa Tanzania – huko Kiabakari – miradi miwili ya maendeleo iliyofadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland katika mashindano ya Polish Development Aid ya 2021 na kutekelezwa na Kiabakari Foundation pamoja na Parokia ya Kikatoliki ya Kiabakari imezinduliwa.
-
25.03.2022Tamasha la Wasanii wa Poland na Tanzania wakati wa Toleo la Pili la Tamasha la Pamoja ZanzibarMnamo Machi 23, 2022, katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam, tulifurahi kusikiliza tamasha la wasanii wa Poland na Tanzania ikiwa ni sehemu ya tamasha la 2 la Pamoja Zanzibar, lililoandaliwa na Radek Bond Bednarz na kuungwa mkono na Ubalozi wetu. Balozi Buzalski alijitolea tamasha kwa ajiri ya wahasiriwa wa vita huko Ukraine.