Habari
-
21.01.2022Tunafanya kazi kuongeza ujasiriamali wa wakazi wa Usandawe na kulinda sanaa ya miamba katika Hifadhi ya Swaga SwagaShukrani kwa ushiriki wa mwanaakiolojia wa Poland Maciej Grzelczyk na ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa mwaka 2021 mradi uliotekelezwa kama sehemu ya misaada ya Kipolandi yenye lengo la kuamsha na kuelimisha wakazi wa eneo la Usandawe nchini Tanzania kwa ajili ya kulinda sanaa ya miamba na urithi wa kitamaduni wa jamii ya Wasandawe umekamilika.
-
28.12.2021Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam utafungwa Januari 6-7, 2022Tunapenda kuwafahamisha kuwa ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam utafungwa tarehe 6-7 Januari 2022.
-
28.12.2021Makaburi mengine ya Poland nchini Tanzania - huko Kidugala - yamekarabatiwaShukrania kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam, kituo cha nyaraka,ufukuzwaji na uhamisho wa Chuo Kikuu cha Pedagogical huko Cracow,wakfu wa PU “pro Univesitatis” na Wizara ya Utamaduni na Urithi wa kitaifa, makaburi mengine ya Poland nchini Tanzania yamekaratiwa.
-
09.12.2021Shukrani kwa Mfuko wa Msaada wa Poland, Watoto kutoka katika Milima ya Usambara tayari wanafaidika na chumba cha pili cha ziada cha mtaala wa kawaidaMwaka huu, Shukrani kwa ushiriki wa mshirika wa ndani -A.D. Views Management Ltd. na fedha zilizochangwa kama sehemu ya ushirikiano wa maendeleo wa Poland na Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam, tayari takribani wasichana na wavulana 300 kutoka wilaya ya Lushoto katika milima ya Usambara kaskazini mwa Tanzania wanahudhuria vyumba vilivyopangwa maalum vinavyotoa sio tu mahali salama pa kucheza, lakini juu ya yote kujifunza.
-
05.12.2021Mfuko wa misaada wa Poland kuendelea kuisaidia Tanzania katika mapambano yake dhidi ya Kifua KikuuUlinzi wa afya ni mojawapo ya vipaumbele vya ushirikiano wa maendeleo wa Poland na nchi za Afrika. Ndio maana mwaka huu tunaendelea kufadhili mradi wa shirika la APOPO unaotekelezwa nchini Tanzania, unaojumuisha kugundua ugonjwa wa kifua kikuu kwa msaada wa panya wakubwa wa kusini.
-
25.11.2021Tamasha la piano kwenye hafla ya Mwaka wa ChopinKama sehemu ya kusherehekea Mwaka wa Chopin, tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2021, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es salaam uliandaa tamasha la piano kwa ushirikiano na Ubalozi wa Ujerumani lililochezwa na mpiga kinanda mahiri wa Poland Jan Krzysztof Broja.
-
12.11.2021Tuliadhimisha Siku ya Uhuru waTanzaniaWakati wa tafrija ya sherehe za kuadhimisha miaka 103 ya kupata uhuru iliyoandaliwa katika bustani za ubalozi wa Jamhuri Poland jijini Dar es salaam, Balozi Krzysztof Buzalski alisoma barua kutoka kwa Waziri SzymonSzynkowskivelSęk yenye kuwatakia kheri wanadiaspora wa Poland duniani na alikumbuka historia ya kurejesha uhuru.
-
01.11.2021Ziara ya Siku ya Watakatifu Wote katika makaburi ya Tengeru na KinondoniSiku ya Watakatifu wote ilikua ni hafla ya kuwakumbuka watu waliohamishwa kutoka Poland kutokana na Vita vya Pili vya Dunia nchini Tanzania. Balozi Krzystof Buzalski pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Utamaduni na Urithi wa Taifa waliweka shada la maua katika makaburi ya Tengeru, na wawakilishi wengine wa ubalozi walitembelea makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
-
29.10.2021Onyesho la filamu ya “Sweat” katika Tamasha la Filamu la UlayaIkiwa ni sehemu ya Tamasha la Filamu la Ulaya, lililoungana na Tamasha la Kimataifa la Filamu visiwani Zanzibar, Oktoba 29, 2021, Ubalozi wa Jamhuri ya Poland jijini Dar es Salaam uliandaa onyesho la filamu iliyoshinda tuzo. “Sweat” katika Taasisi ya Ufaransa iliyopo nchini Tanzania.
-
22.10.2021Shukrani kwa msaada wa Wapoland, Tunaandaa jengo jipya la Chekechea- ‘Holy Family Day Care’ huko SegereaFenicha mpya za shule, magodoro pamoja na jiko, vifaa vya kufulia na uwanja wa michezo vitahudumia watoto wadogo kutoka Segerea hivi karibuni, Wilaya ya Dar es Salaam, pamoja na wafanyakazi wa shule wanaofanya kazi katika shule ya chekechea. Ununuzi wa vitu vya msaada wa Poland utawawezesha Masista Wamisionari wa Familia Takatifu kufungua hivi karibuni jengo jipya la Chekechea-Holy Family Day Care.